Home BIASHARA Fanya haya, Kabla ya kutafuta muwekezaji.

Fanya haya, Kabla ya kutafuta muwekezaji.

0 comment 231 views

Katika kuanzisha biashara, mara nyingine mmiliki anajikuta na uhitaji mkubwa wa muwekezaji. Hii inaweza kusababishwa na masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya mtaji. Kama kuna uwezekano wa kufanya hivyo, ni hatua nzuri kwa kuwa inakupeleka mbele zaidi. Lakini kabla ya kutafuta muwekezaji kwa ajili ya biashara au kampuni yako unapaswa kujiuliza: Je, huu ni wakati sahihi wa kuchukua hatua hiyo?

Yafuatayo ni mambo matatu ambayo unapaswa kujiuliza kabla ya kuchukua uamuzi wa kutafuta wawekezaji.

  • Umetumia rasilimali zako zote?

Umehakikisha kuwa umefanya kila kitu kilihopo ndani ya uwezo wako? Umepata muelekeo sahihi wa biashara yako kabla ya kumuingiza mtu mwingine ambaye atakuja na mawazo na muelekeo tofauti kabisa na wa kwako? Kampuni au biashara yako ikiwa na thamani ya juu kabla ya kukutana na wawekezaji, unakuwa katika nafasi nzuri zaidi wakati wa majadiliano.

  • Una nini zaidi ya wazo zuri?

Kama ulichonacho ni wazo zuri la biashara pamoja na ubunifu, ni vizuri kutotafuta wawekezaji mara moja kwani katika hatua hiyo, watataka kuongoza kila kitu katika masuala ya umiliki hivyo nafasi yako katika kuendesha biashara na kufanya maamuzi itakuwa ndogo sana. Kabla ya hatua ya kutafuta wawekezaji, hakikisha umejipanga ili kuwaonyesha kuwa una uwezo wa kuendesha biashara au kampuni hiyo na kuleta mafanikio.

  • Hakikisha muwekezaji anaelewa malengo yako

Ni muhimu kuhakikisha kuwa muwekezaji anaelewa vuzuri biashara yako, malengo yako ya baadae na muda ambao umeweka kwa ajili ya mchakato mzima. Muwekezaji ambaye atakubali kuwekeza bila kuelewa wazo lako la biashara kwa kina anaweza kupata wasiwasi pale ambayo mipango itaenda yofauti na matarajio yako hivuo kuamua kuachana na biashara hiyo na kukurudisha hatua kumi nyuma.

Ukizingatia haya, bila shaka utapata muwekezaji sahihi katika biashara au kampuni yako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter