Home BIASHARA Huduma za bidhaa mtandaoni, biashara inayokua kwa kasi

Huduma za bidhaa mtandaoni, biashara inayokua kwa kasi

0 comment 106 views

Kuna maisha baada ya Jumia, Jumia ilikuwa ndio mtandao mkubwa kwa Tanzania kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao na sasa huduma hiyo haipo tena.

Mwishoni wa mwaka 2019, Jumia ilisitisha shughuli zake nchini na tunaweza kusema manunuzi kupitia njia ya mtandao yameshuka ama kupungua kabisa.

Jumia ambayo ilikuwa biashara ya mtandao nchini haipo tena ikiwaaacha watanzania wengi wa manunuzi ya mtandaoni bila huduma hiyo. Takribani asilimia 15 ya watu nchini wanatumia intaneti hivyo kuna wanunuzi wengi wa njia ya mtandao. (online)

Ni nini umuhimu wa biashara ya mtandao Tanzania, ama kuwa na uwezo wa kuagiza mahitaji yako ya kila siku kupitia kiganjani mwako na kuletewa mlangoni mwako? Ni mkubwa sana.

Hii imebaki kuwa sekta kubwa ambayo haijaguswa ipasavyo na inafanywa na wachache na matokeo yake ni kwamba serikali inapoteza mapato na walaji wanaachwa bila huduma.

QNET ni biashara ya mtandao ambayo imejikita katika mauzo ya moja kwa moja ambayo imevutiwa kuziba pengo hilo na kuziba mapengo katika biashara hii ya mtandao.

Ni kweli, biashara ya mtandao nchini Tanzania bado iko katika hatua ya maendeleo, hata hivyo bila shaka inauwezo wa kukua haraka.

Ikiwa mahitaji ya huduma hii ni makubwa, bado kuna shida ambapo Watanzania wana mashaka sana na biashara hii.

Kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao bado ni tatizo kwa sasa.

Hii ilipelekea Jumia kuondoka na ndio sababu wafanya biashara ya mtandao wa dunia kama QNET kuingia.

Hata hivo, kukosekana kwa mipango miji mizuri, kunafanya kukosekana kwa anwani sahihi za uwasilishaji wa bidhaa, kutoaminika kwa wauzaji wa mtandaoni na ukuaji wa biashara hii katika soko hili kubwa.

Ifahamike kwamba, Tanzania ni ya nne barani Afrika kwa biashara ya mtandao yenye watumiaji wanaokadiriwa kuwa milioni 1,593, hii ni kwa mujibu wa Kielelezo cha Biashara ya mtandao cha UNCTAD. UNCTAD imeiweka Tanzania nafasi ya pili baada ya Kenya katika biashara ya mtandao.

“Ingawa hakuna takwimu zinazoonyesha kiasi cha mauzo ya mtandaoni, miamala ya simu milioni 1,4446 yenye thamani ya dola za Marekani 21.73 bilioni ilifanyika kati ya July 2016 na April 2017,” inaripoti Benki Kuu ya Tanzania.

Kampuni ya biashara ya mtandao QNET, yenye uzoefu na uwepo mkubwa Afrika Magharibi inatoa suluhisho la kipekee haswa baada ya kuzuka kwa janga la Covid-19.

Tanzania ni taifa linaloendelea, kutokana na ukosefu wa miundombinu haswa katika miji mingi, inafanya QNET kukabiliwa na changamoto kubwa katika kukuza soko hili na kutimiza mahitaji ya wengi.

Kampuni kama QNET na iliyokuwa Jumia ndio suluhisho. Kwa mfano Amazon, tayari imepenya Afrika Kusini.

The Mall of Africa iliyopo nchini Nigeria ni mall ya mtandaoni ambayo inajipanua Afrika Magharibi. Alibaba pia inaongoza Afrika na Kilimall nchini Kenya.

Tanzania ikiwa katika hatua za kupunguza umaskini kwa kuboresha maisha, na idadi kubwa ya watu wakiwa wanaishi vijijini,biashara ya mtandao kupitia njia ya kuuza moja kwa moja inatoa suluhisho hilo.

Uwezo wa kuuza na kununua kwa njia ya mtandao inasaidia bidhaa kufikishwa kwa mlaji hususani katika maeneo yasiyofikika.

Kimsingi, uuzaji wa moja kwa moja hutumia fursa ya kuuza bidhaa na huduma moja kwa moja kwa watumiaji, popote walipo.

Tatizo sio tuu kupata huduma na bidhaa, bali ni kuwa na uhakika ni wapi bidhaa hiyo inatoka na uhakika wa kumfikia mnunuzi.

Ili kuelewa vizuri mchakato huo, bidhaa huagizwa katika mtandao wa QNET kupitia mshirika ambae huwasilisha bidhaa hizo. Hii inafanya biashara kuwa urahisi kwa pande zote mbili yaani mnunuzi na muuzaji.

Kupitia biashara ya mtandao, wafanyabiashara wanapata fursa ya kuuza na kuongeza mauzo ya bidhaa zao na kuwafanya wanunuzi kupata huduma kwa viwango vya kimataifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter