Home BIASHARA JIFUNZE NJIA UNAWEZA KUTUMIA KUPATA WAZO LA BIASHARA

JIFUNZE NJIA UNAWEZA KUTUMIA KUPATA WAZO LA BIASHARA

0 comment 74 views


1. TUMIA UJUZI ULIO NAO

Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, kwanini usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari kwanini usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wanakuja huko kuogelea?

Kama unapenda bustani unaweza anza biashara ya kufanya bustani.

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupata wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizi kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Bidhaa Maarufu na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna masharti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na bidhaa yenyewe, nah ii ni maharufu sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, maduka makubwa NA MADUKA MENGINE.

Na usijalibu kutumia Bidhaa ya kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa maana inaweza kukuletea shida na ukajikuta unafilisiwa.

5. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe.

-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
– Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

6. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

7. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.

8. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.

9. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

10. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara
11. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
– Maonyesho ya biashara
– Magazeti,
– Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
– Kwa marafiki.

12. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter