Home BIASHARA Jinsi ya kuwasiliana na Mteja aliyekasirika/kutofurahishwa na huduma

Jinsi ya kuwasiliana na Mteja aliyekasirika/kutofurahishwa na huduma

0 comment 74 views

Katika biashara huwa kuna changamoto nyingi ambazo Mfanyabiashara hukumbana nazo. Kikawaida Mteja ni mfalme hivyo hata kama atakuudhi kwa namna yeyote wewe kama mfanyabiashara unatakiwa kujishusha ili mwisho wa siku uweze kuuza bidhaa au huduma yako na kujiongezea kipato.

Si rahisi kwa kila mfanyabiashara kuvumilia mfarakano baina yake na mteja, lakini Mfanyabiashara anatakiwa kuzingatia malengo aliyo nayo kuhusu biashara yake . Hivyo basi zifuatazo  ni baadhi ya namna ambazo zinaweza kumsaidia mfanyabiashara au mjasiriamali kuwasiliana na mteja aliyekasirika/kutofurahia huduma:

Kuwa Mtulivu. Siku zote mteja asipofurahishwa na huduma huanza kutumia lugha zisizofaa na muda mwingine anaweza kumpazia sauti mfanyabiashara. Ili kuondokana na mfarakano zaidi wewe kama mfanyabiashara unashauriwa kuwa mtulivu hii itamsaidia hata mteja kuona kwamba hakuna umuhimu wa kupaza sauti hivyo kumfanya na yeye aweze kutulia kwa kiasi fulani ili kufikia muafaka kuhusu tatizo.

Usichukulie binafsi hasira za mteja. Unapaswa kukumbuka kwamba mteja hana hasira na wewe moja kwa moja bali ana hasira na bidhaa, au huduma katika biashara yako. Hivyo hata maamuzi yako yanapaswa kulenga biashara yako sio wewe binafsi.

Jitahidi kutumia ujuzi wako wa hali ya juu kumsikiliza mteja. Mteja mwenye hasira siku zote huhitaji kusikilizwa. Hivyo kwa namna yeyote hutegemea mwenye biashara kumsikiliza hivyo unashauriwa kusikiliza kwa makini kabla ya kufanya maamuzi ya kusuluhisha tatizo. Lugha ya mwili ni muhimu sana ukiwa unamsikiliza mteja kwasababu matendo yako utakayofanya unavyomsikiliza yanaweza kuongeza hasira au kupunguza hasira za mteja. Kwamfano yeye anajieleza wewe uko bize unaandika au unatumia simu, hii si sahihi jitahidi kumuangalia usoni ili ajue kwamba unasikiliza na una mpango wa kutoa suluhisho.

Baada ya kumsikiliza, muonyeshe mteja kwamba unamuonea huruma na unaelewa jinsi anavyojiskia kuhusu tukio au changamoto aliyoipata. Hii itamfanya mteja kujisikia vizuri na kuona kuwa unawaheshimu na kuwajali wateja wako.

Muombe msamaha Mteja hata kama malalamiko yake hayaleti maana sana. ni muhimu kumuomba msamaha mtaje. Kwasababu hapa unataka aendelee kuwa mteja katika biashara yako. Si lazima ujielezee sana hapa. Kwamfano unaweza kusema “ samahani sana kwa kutofurahishwa na huduma/bidhaa yetu, hebu tuone nini tunaweza kufanya ili kusuluhisha tatizo hili”

Tafuta suluhisho. Mara nyingi mteja hulalamika kwasababu anataka njia mbadala ipatikane kusuluhisha changamoto aliyokumbana nayo katika biashara yako. Hivyo unaweza kumuuliza nini kifanyike ili kuondoa tatizo hilo na kumfanya ajisikie vizuri. Kama jambo atakalosema linaweza kufanyika basi mfanyie, kama ni nje ya uwezo wako unaweza kutoa wazo jingine linaloendana na anachotaka ili kumridhisha.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter