Home BIASHARA Kila biashara inahitaji mitandao ya kijamii

Kila biashara inahitaji mitandao ya kijamii

0 comments 169 views

Kila biashara huwa makini na sehemu ambazo wanawekeza fedha kwa ajili ya kutafuta wateja hasa ikiwa wana bajeti ndogo. Lakini teknolojia na utandawazi umesaidia wafanyabiashara wengi katika hili ambapo mbali na kulipia matangazo katika televisheni, redio, na magazeti sasa kuna mitandao ya kijamii ambayo wafanyabiashara wanaweza kutangaza bidhaa na huduma zao. Hivyo basi kama mfanyabiashara ni muhimu kujihusisha na mitandao ili kuweza kuitangaza biashara yako na kujipatia wateja zaidi.

Siku hizi watu wengi wanatumia mitandao mbalimbali ya kijamii, inaelezwa kuwa zaidi ya 59% ya watu hutumia mitandao ya kijamii kila siku. Hivyo kwa kuitangaza biashara yako katika mitandao ya kijamii moja kwa moja unakuwa unajihusisha na watu wa aina mbalimbali hivyo kupelekea kupata wateja wengi wa kununua bidhaa kwako. Ni muhimu kwa kila mjasiriamali kutangaza biashara yake katika mitandaoni ili kupata wateja kwa urahisi.

Kupitia mitandao ya kijamii mfanyabiashara anapata nafasi ya kujitangaza, jambo ambalo litawafanya wafuatiliaji wake kuona utofauti wa biashara hiyo na biashara nyingine na kuchukua hatua ya kununua bidhaa au huduma husika. Pia kupitia mitandao ya kijamii unawarahisishia wateja kujua taarifa fupi kuhusu bidhaa au huduma yako. Ikiwa unataka kukuza biashara yako hakikisha kila kitu unachoweka katika akaunti yako kitawahamasisha wateja zaidi.

Mitandao ya jamii ni gharama nafuu zaidi katika upande wa matangazo ikilinganishwa na televisheni, redio, na magazeti. Unaweza kutangaza biashara yako hata ukiwa na 10,000 katika mitandao ya kijamii jambo ambalo haliwezekani katika vyombo vya habari. Tambua ni watu gani unataka kuwauzia bidhaa zako, tengeneza bajeti na kisha weka jitihada kubwa katika kujitangaza na kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia mitandao ya kijamii.

Inaelezwa kuwa wateja wengi hupendelea kuwasiliana, kuuliza maswali nk kupitia mitandao ya kijamii na kupata mrejesho wa haraka. Pia ni rahisi kwa mteja kununua bidhaa au huduma ikiwa atawasiliana kwa urahisi na mfanyabiashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!