Home BIASHARA Korosho ni mapatano- Manyanya

Korosho ni mapatano- Manyanya

0 comment 101 views

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema bungeni Dodoma kuwa serikali haijapanga bei maalum ya korosho ghafi hivyo biashara hiyo ni makubaliano baina ya mfanyabiashara na mnunuzi. Manyanya amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe aliyetakaserikali kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu kiwango kilichoelekezwa katika uuzaji wa korosho ghafi na zile zilizobanguliwa.

“Kwanza niseme kuwa hadi sasa serikali inazo tani 361 za korosho, hivyo wanunuzi wanakaribishwa lakini hatuna bei maalumu ya kiasi gani tunaziuza bali tunafanya mapatano”. Ameeleza Naibu Waziri huyo.

Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Silafi Maufi amehoji kuhusu mkakati wa serikali katika kujenga viwanda au kupeleka wawekezaji ambao watajenga viwanda vikubwa mkoani Rukwa kwa lengo la kuanzisha ajira. Pia amehoji suala la mazao ya mkoani humo kupewa bei holela, jambo linalopelekea maisha ya wananchi kuwa magumu.

katika maelezo yake, Naibu Manyanya amesema kuwa kwa sasa kilimo cha mkataba kinatumika katika mazao mbalimbali kama tumbaku na miwa ili kurahisisha makubaliano baina ya mkulima na mnunuzi. Kuhusu viwanda, amesema kuwa serikali imejikita katika kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter