Home BIASHARA Maboresho Bandari ya Tanga yavutia wafanyabiashara

Maboresho Bandari ya Tanga yavutia wafanyabiashara

0 comment 147 views

Baada ya kufanyika mkutano wa siku moja kati ya uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha, imeelezwa kuwa, wafanyabiashara kutoka kanda ya kaskazini wameonyesha dhamira ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kwa ajili ya kupitisha shehena ya mizigo yao, kufuatia kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji.

Meneja wa Bandari ya Tanga, Percival Salama ameeleza kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake, miundombinu, mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo imeboreshwa ambapo kwa sasa, taratibu za kuchukua mizigo zinatumia muda mchache tofauti na hali ilivyokuwa hapo mwanzo.

“Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi bandari ya Tanga ni nzuri, salama kwa mizigo na ni ya uhakika kwa vile tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi, miundombinu, utendaji kazi na Tehama. Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu”. Amesema Salama.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Lydia Mallya ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia bandari hiyo kwani inakidhi viwango vya kimataifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter