Home BIASHARA Majaliwa: Wafanyabiashara msikubali kutoa rushwa

Majaliwa: Wafanyabiashara msikubali kutoa rushwa

0 comment 81 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na wafanyabiashara Kariakoo jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa wafanyabiashara hao kutotoa rushwa kwa chombo chochote kwani serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kukemea vitendo vya rushwa. Majaliwa amewaambia wafanyabishara hao kuwa, endapo wataona mazingira ya rushwa, wasisite kutoa taarifa kwani rushwa ni adui wa haki.

“Rushwa si sehemu ya mkakati wa serikali, hivyo vita dhidi ya rushwa lazima iendelezwe na watu wote. Mafanikio tuliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa huduma za afya ni matokeo ya kupiga vita rushwa”. Amesema Waziri Mkuu.

Katika mkutano huo, Majaliwa amesema serikali inapanga kubadilisha utaratibu wa kufanya biashara Kariakoo ili wafanyabiashara waweze kufanya shughuli zao kwa masaa 24 kama ilivyo kwa masoko makubwa kote duniani. Waziri huyo amesema lengo la mabadiliko hayo ni kukuza uchumi wa wafanyabiashara na wa taifa kwa ujumla.

“Nchi yetu ina usalama na ulinzi wa kutosha hivyo hatuwezi kushindwa kufanya biashara wakati wote”. Ameeleza Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Dar es salaam ndio jiji la kibiashara nchini, hivyo serikali inafanya jitihada zote kuboresha mwenendo wa biashara na kutoa fursa zaidi kwa wafanyabiashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter