Home BIASHARA Maziwa ya Azam kurudi sokoni

Maziwa ya Azam kurudi sokoni

0 comment 154 views

Baada ya maziwa ya Azam kutoweka kwenye masoko Tanzania Bara kwa takribani miezi sita kutokana na tozo kubwa, serikali imeingia makubaliano na kampuni hiyo ili kuweza kurejesha bidhaa hiyo sokoni. Kanuni ya Wizara ya Uvuvi na Mifugo ilikuwa ikiwaelekeza Azam kulipa Shilingi 2,000 kwa kila lita ya maziwa kutoka Zanzibar, jambo ambalo liliwashinda na hivyo kuacha kusafirisha maziwa lakini baada ya kufanya mazungumzo, Azam wamepewa masharti kadhaa na tozo hizo zimepunguzwa hadi Sh. 250 kwa lita.

Msajili wa Bodi ya Maziwa (TDB) Dk. Sophia Mlote amesema kuwa serikali inaitaka Azam Dairies kujenga kiwanda cha maziwa Tanzania Bara ili watanzania waweze kunufaika. Vilevile, Azam Dairies wametakiwa kununua maziwa yake katika Ranchi ya Taifa (Narco).

“Tunahitaji waendelee kufanya biashara kwa faida ya taifa ikiwamo kuongeza ajira na soko la maziwa kwa wafugaji”. Amesema Mlote.

Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania haizalishi lita nyingi za maziwa kama inavyotakiwa kutokana na ukosefu wa malighafi na teknolojia. Imeelezwa kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, maziwa yanayotakiwa kuzalishwa ni lita bilioni 11 lakini viwanda huzalisha lita bilioni 2.4 pekee na kusindika lita 150,000 badala ya lita 750,000 kwa siku.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter