Home BIASHARA Ongeza mauzo yako, zingatia haya

Ongeza mauzo yako, zingatia haya

0 comment 105 views

Watu wengi hukimbilia kufanya biashara bila kuwa na mpango maalum utakaowapa muongozo na hii hupelekea biashara nyingi kufungwa muda mfupi tu baada ya kuanzishwa. Ukweli ni kwamba, ni muhimu kujipanga kama unataka biashara yako izae matunda. Huwezi kupata mafanikio kirahisi bila kuwekeza chochote.

Kuna mambo ya msingi ambayo mfanyabiashara anatakiwa kuyafahamu ili kutimiza malengo yake. Lengo hapa sio kuongeza mapato peke yake bali ni kuhakikisha shughuli unayofanya inazalisha faida. Kuna wafanyabiashara ambao wameshuhudia bidhaa zao zikiendelea kufanya vibaya sokoni kutokana na kushindwa kuzingatia misingi muhimu ambayo imesaidia wengine kufanikiwa.

Mfanyabiashara unapaswa kuzingatia haya ili kuipelekea biashara yako mbali na hatimaye kufanikiwa:

  • Unatakiwa kuelewa mbinu za kufanya biashara kwa kutumia mitandao ya kijamii. Kama mfanyabiashara, unatakiwa kuwa na mfumo thabiti ambao utakuwezesha kuingiza kipato hata unapokuwa nyumbani. Dunia hivo sasa ipo kiganjani hivyo watu hutafuta mahitaji yao ya kila siku kupitia mitandao ya kijamii. Ni muhimu kujifunza mbinu za kufanya biashara mtandaoni.
  • Hakikisha wewe ni mtaalamu wa biashara unayofanya. Unapofahamu biashara yako kwa undani, inakuwa rahisi kuizungumzia na kumshawishi mteja. Ili kuinua kipato chako, ni vizuri kuwa na ujuzi, ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu huduma au bidhaa unayoweka sokoni.
  • Huduma bora kwa wateja. Wekeza katika utoaji bora wa huduma na mfanye mteja ashawishike kurudi tena kwa mara ya pili. Hakuna mteja atakayerudi kwako kama huduma ikiwa mbovu. Ubora wa huduma ni kivutio kikubwa katika biashara.
  • Ni muhimu kusikiliza na kufanyia kazi maoni pamoja na ushauri unaopewa. Ikiwa wewe ni mtu usiyependa kuwasikiliza wengine, itakuwa ngumu kuona muelekeo wa biashara yako na kujua ni nini hasa wateja wako wanategemea kutoka kwako.
  • Fanya kazi kwa bidii bila kuchoka. Usiruhusu changamoto zikukatishe tamaa na badala yake, zitumie kujifunza na kufanya mabadiliko yatakayoleta matokeo mazuri.

Katika biashara yoyote ile, vitu vya msingi vinavyopeleka kufanya vizuri sokoni na kupata wateja wengi ni huduma bora, mawasiliano, mazingira rafiki na kuendelea kujifunza kila siku.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter