Home BIASHARA Petroli yaadimika Zanzibar

Petroli yaadimika Zanzibar

0 comment 123 views

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar, Haji Kali Haji amethibitisha kuwa mafuta aina ya petroli yamepungua visiwani humo. Haji ameeleza kuwa sababu ya mafuta hayo kuadimika ni kampuni ya United Petroleum kuchelewesha kuingiza mafuta hayo kisiwani humo kwa wakati uliopangwa.

Hadi sasa kampuni ya Zanzibar Petroleum na Gapco ndio pekee zilizoweza kuingiza mafuta Zanzibar ambapo Gapco ina kiwango cha mafuta lita 942,317 ya petroli, dizeli lita 799,629 na mafuta ya taa lita 213,305. Kwa upande wa Zanzibar Petroleum, wana mafuta lita 407,415 za petroli, dizeli lita 904,488, na mafuta ya taa lita 215,912. Kampuni ya United Petroleum wana akiba ya petroli lita 98,152, dizeli 205,505 na mafuta ya taa lita 472,194.

Kampuni ya Zanzibar Petroleum inategemea kuingiza mafuta lita 1,600,000 ya petroli hapo Machi 10 mwaka huu kwa kutumia meli iitwayo East Wind I. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, kampuni ya United Petroleum imetozwa faini ya Dola za kimarekani 20,000 kwa kuchelewesha kuingiza mafuta hayo na kuagizwa kulipa ndani ya wiki mbili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter