Home BIASHARA Rais Samia azungumza na Dangote

Rais Samia azungumza na Dangote

0 comment 73 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na mfanyabiashara ambaye pia ni Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu,   Gerson Msigwa imesema Alhaji Dangote amempongeza Rais Samia kwa kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Taarifa hiyo imesema Alhaji Dangote amemuahidi Rais Samia kuwa kampuni yake iliyowekeza zaidi ya Sh1.76 trilioni, itaendelea kuwekeza katika maeneo mengine ukiwemo mpango wa kujenga kiwanda cha mbolea.

“Tutaendeea kuwekeza Tanzania ili kuzalisha ajira, mapato ya nchi na kuinua ustawi wa wananchi, nadhani anahitaji kuungwa mkono katika hili na tumemuahidi kuwa tutaendela kuwekeza kwa kiasi kikubwa hapa Tanzania ili kuunga mkono anachofanya, sisi tutazalisha ajira,” amesema Alhaji Dangote.

Dangote amesema kutokana na kubadilika na kuimarika kwa mazingira ya biashara nchini, atawahimiza wafanyabiashara na wawekezaji wenzake kuwekeza Tanzania kwa kuwa serikali ipo tayari kushirikiana nao.

Kwa upande wake Rais Samia, amempongeza Dangote kwa uwekezaji alioufanya hapa nchi na amemhakikishia kuwa serikali itahakikisha uwekezaji wake na wawekezaji wengine unalindwa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Rais pia amewaagiza Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Masauni ambao wamehudhuria mazungumzo hayo kufanyia kazi changamoto zote zinazokikabili kiwanda cha Dangote ili kiendelee kuzalisha inavotakikana na kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter