Home BIASHARA Serikali kuendelea kupigania PSDS

Serikali kuendelea kupigania PSDS

0 comment 114 views

MKUU wa Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Ezamo Maponde amesema serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuwezesha mkakati wa maendeleo ya sekta binafsi katika nchi za Afrika Mashariki (PSDS) kufanikiwa.

Aidha alisema, serikali imekuwa mstari wa mbele kufanya mabadiliko mbalimbali ya sera zake ikiwemo mpango wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2015 ili kusukuma mbele sekta za Kilimo na biashara.

Alisema hayo wakati wa kufunga kwa mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki , mradi uliokuwa ukiratibiwa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Sera, Uratibu na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu alisema kutokana na mabadiliko ya kisera na usimamizi wa utekelezaji wake Tanzania imefanikiwa kujiondoa katika utegemezi.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Ezamo Maponde akizungumza wakati wa kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema juhudi zilizofanyika kuweka msingi katika mradi huo kutatochoea kuimarishwa kwa Kilimo na kuwa na Kilimo biashara ili ndoto za kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda kufanikiwa.

Alisema kutokana na haja hiyo serikali imekuwa ikitengeneza sera na kubadili kanuni mbalimbali ili  kuhimiza uchumi wa kiushindani wa viwanda toka mwaka 1961 kwa lengo la kupunguza utegemezi katika bajeti. Sekta ya viwanda nchini imegawanyika katika maeneo matatu ya uzalishaji (53%) uchakataji (24 %) na uunganishaji (4%).

Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea mazao ya Kilimo kinachoajiri asilimia 75 ya wananchi, ndio nguzo ya uzalishaji wa bidhaa katika viwanda.

Kutokana na utegemezi huo viwanda vinavyochakata mazao ya Kilimo hasa chakula ni asilimia 24, viwanda vya nguyo na nyuzi asilimia 10 na kemikali asilimia 8.5.

Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dk. Tausi Kida wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mradi huo Profesa Fortunata Makene, Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) alisema kwa kiasi kikubwa umesaidia katika kuleta tija katika sekta ya kilimo na biashara ikiwemo kuzishawishi serikali kufanya mabadiliko katika sera zake.

Akizungumza katika mkutano  huo uliowakutanisha  wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara kujadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu  kuzinduliwa kwake, alisema mradi huo uliokuwa na lengo la kuzishawishi serikali katika masuala ya sera kupitia mpango ujulikanao kama ‘National Reference Group’.

Alisema mradi huo ulilenga kuangalia namna ambavyo masuala ya mabadiliko ya tabia nchi  yanahusishwa na shughuli za kilimo na biashara ili kuleta tija kwa wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.

Wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara walioshiriki hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Profesa Makene alisema kimsingi mradi huo uliondeshwa kwa awamu mbili kwa vipindi vya miaka minne minne tangu kuanzishwa kwake umeweza kuchangia mabadiliko hayo  na kuongeza uelewa kwa wadau husika wakiwemo wanawake kutoka vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na kazi za usindikaji wa vyakula na bidhaa

Aidha alisema uwepo wa sera madhubuti katika kilimo na biashara kwa kiasi kikubwa kumeweza kuleta mabadiliko chanya kwa wakulima na wafanyabiashara ikiwemo kuongeza thamani katika mnyororo.

Nchi za Afrika Mashariki kwa sasa zipo katika kuendeleza mpango wa Private Sector Development Strategy (PSDS) 2018-2022 wenye lengo, la kuimarisha mazingira bora ya biashara na kuzifanya kuwa za ushindani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter