Home BIASHARA TBS yashauri wazalishaji kuzingatia ubora, kuuza nje

TBS yashauri wazalishaji kuzingatia ubora, kuuza nje

0 comment 129 views

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Prof. Makenya Maboko ametoa wito kwa wazalishaji wenye leseni za kutumia alama za ubora kutumia fursa hiyo kupanua masoko na kuuza bidhaa zao nje ya nchi. Prof Maboko ameeleza kuwa alama hizo zina umuhimu mkubwa kwa biashara kwani zinampa mzalishaji uhakika kuhusu bidhaa zake na hivyo kumjengea imani kwa wateja,

“Lakini pia alama ya ubora humsaidia mzalishaji kupanua masoko ya bidhaa zake nje ya nchi na ni wazi basi hatua hii ni ya kujivunia sana kama mzalishaji na kama taifa kupanuka kwa masoko ya kikanda na kimataifa kutasaidia kuongeza fedha za kigeni, hivyo kusaidia kukuza uchumi”. Amesema Mwenyekiti huyo.

Pamoja na hayo, Prof. Maboko amewataka wamiliki wa leseni hizo kuzingatia masharti wakati wa uzalishaji na kuhakikisha bidhaa zao zinakidhi viwango na kueleza kuwa, kufanya hivyo kutasaidia ukuaji wa uchumi sio tu kwa wazalishaji hao bali kwa taifa kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter