Ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) imerejesha safari zake za moja kwa moja kutoka Istanbul hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA).
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema “kwa upande wa Serikali tunayo furaha kubwa sana kuona hizi kampuni kubwa za ndege zinarejesha safari zake hapa nchini Tanzania katika vituo mbalimbali.
Tafsiri yake ni moja tuu kwamba idadi ya wageni wanaokuja nchini kwetu wengi wao wakiwa ni watalii inaongezeka.”
Kwa hapa KIA kuwaona Turkish Airline wakirejea katika safari za moja kwa moja inaongeza kwenye safari walizokuwa wakizifanya kati ya Istanbul na Dar es Salaam, sasa watakuwa wakifanya safari nne kutoka Istanbul hadi KIA na kutoka KIA kwenda Zanzibar.
Amesema ujio wa ndege hiyo umechangiwa na filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema Turkish ni kampuni kubwa barani Ulaya hivyo ujio wake utaiunganisha Tanzania na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Ameeleza kuwa kwa upande wa Serikali unachagiza utekekezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza kufikia watalii milioni tano ifikapo 2025
Ndege hizi zitakuwa zikifanya safari nne kwa wiki zikitumia ndege aina ya Airbus A330-300 zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 289 kwa mara moja.
Kampuni hiyo ina ndege zaidi ya 370.