Home BIASHARA Unachotakiwa kufanya kuimarisha biashara

Unachotakiwa kufanya kuimarisha biashara

0 comment 99 views

Ni muhimu kwa kila biashara kutengeneza jina tangu mwanzo ili kuepuka kuwachanganya wateja kuhusu huduma au bidhaa inayopatikana. Jambo la msingi linaloweza kukusaidia kufanikisha hili ni pamoja na kujua aina ya wateja unaotaka kuwauzia huduma au bidhaa yako.

Badala ya kujihusisha na wateja wa aina mbalimbali, jitahidi kujihusisha na wateja wa aina moja ili kurahisisha mahusiano baina ya kampuni na wateja. Pia kwa kujihusisha na kundi maalum itakuwa rahisi hata kujitangaza na kuwafikia wateja kwa urahisi.

Hivyo basi jiulize, wateja wako:

  • Ni wakina nani?

Tumia muda kujua wateja unaotaka. Mara nyingi ni vyema kufahamu wateja wako wengi wana miaka kuanzia mingapi? Pia ni muhimu kujua jinsia inayoongoza kununua bidhaa zako.

  • Wanapendelea nini?

Si vibaya kufanya utafiti kuhusu mambo ambayo wateja wako wanayapendelea ikiwa ni pamoja na maisha ya kazini na baada ya kazi ili kujua bidhaa zako zina nafasi gani katika maisha yao na zinawasaidia kwa kiasi gani.

  • Wanahitaji nini?

Jifunze kutokana na changamoto ambazo wateja wako wanaweza kuwa wanapitia. Hii itakusaidia kujua kama kuna njia ya kuwarahisishia mapito hayo au kama kuna umuhimu wa kuboresha bidhaa yako ili kuhakikisha wateja wanapata kilicho bora zaidi.

Jambo la msingi ni kutengeneza jina ambalo wateja wanaweza kujihusisha nalo katika maisha yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo. Siku zote watu huvutiwa na bidhaa au huduma ambayo wanaihitaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter