Home BIASHARA Unataka kuanzisha duka la rejareja?

Unataka kuanzisha duka la rejareja?

0 comment 504 views

Watu wengi hufanya biashara ya bidhaa za rejareja kwa sababu haihitaji mtaji mkubwa sana kama biashara ya bidhaa za jumla. Pia biashara ya bidhaa za reja reja ni rahisi kuuza kwa sababu watu huwa na matumizi nazo katika maisha ya kila siku.

Licha ya urahisi wa kuanzisha biashara hiyo, ni muhimu kuangalia uhitaji wa bidhaa kabla hujaanzisha biashara. Kwa mfano kama unaishi sehemu ambayo sio rahisi kupata huduma ya vitu vidogovidogo basi ni rahisi kufungua duka la bidhaa ambazo watu hutumia kila siku. Kwa kufanya hivyo unakuwa umewasaidia wakazi wa eneo hilo na wewe pia unanufaika kifedha.

Pia kufanya biashara ya bidhaa za reja eja kunampa mfanyabiashara uhuru wa kuamua ni bidhaa gani ataziweka katika duka lake na zipi hatoziweka. Ingawa unashauriwa kusikiliza mahitaji ya wateja wako. Biashara inapaswa kuendana na uhitaji wa bidhaa.

Jambo zuri kuhusu biashara ya rejareja, mfanyabiashara ana uwezo wa kuwasaidia wajasiriamali wadogo zaidi. Kwa kufanya maelewano nao ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu kuweka bidhaa zao kwa mfano, mbogamboga, matunda, tambi, ubuyu n.k na iwapo mfanyabiashara atauza kwa niaba ya yao basi anaweza kutengeneza kipato cha ziada.

Mfanyabiashara wa rejareja anatakiwa kujua kuwa jambo lolote linalohusu biashara yake yeye ni mtatuzi. Hivyo kama haupo tayari kutatua matatizo katika biashara hii ni vyema usifungue. Katika kila jambo huwa kunakuwa na changamoto na hivyo hata katika biashara hii changamoto zipo.

Ni muhimu kuangalia wakazi wa eneo unalotaka kufungua biashara kwa sababu unaweza kuona sehemu hakuna maduka ya rejareja na wewe ukaamua kufungua duka katika eneo hilo bila kuangalia aina ya watu wanaoishi katika maeneo hayo. Unaweza kuanzisha duka na kukosa wateja kwa sababu wakazi wa eneo hilo hununua vitu katika maduka makubwa zaidi, na kwa awamu.

Fanya utafiti wa kina kuanzia wakazi wa eneo, bidhaa ambazo zinahitajika kwa wingi pamoja na bei ili kuwa na uhakika wa soko na faida katika baishara yako.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter