Home BIASHARA Unataka kuuza zaidi Instagram? Soma hii

Unataka kuuza zaidi Instagram? Soma hii

0 comment 194 views

Instagram ni moja ya programu ambazo zimekuwa zikikua kwa kasi na kuendelea kupanua upeo wake kila siku. Mwanzo ilianza kama programu ambayo watumiaji wake walikuwa waki ‘post’ picha na video za likizo na maeneo ya starehe , lakini hivi sasa programu hiyo inatumika zaidi kuwahamasisha watu wengine katika masuala mbalimbali, kutangaza biashara na hata kukuza brandi.

Ripoti ya TechCrunch imeeleza kuwa hadi kufikia June 2018 instagram ilikuwa imefikisha watumiaji bilioni 1, huku zaidi ya watumiaji milioni 500 wakitumia programu hiyo kila siku. Hali inayopelekea programu hiyo kuwa moja ya programu maarufu katika jamii ulimwenguni kote

Inaelezwa kuwa, 75% ya watumiaji wa Instagram huchukua hatua, kama vile kutembelea tovuti, au kununua bidhaa baada ya kuona tangazo katika mtandao huo. kutokana na hilo brandi kubwa, wafanyabiashara wa kati na wadogo wote wamekuwa wakitumia Instagram kujitangaza ili kuwafikia wateja wapya na hata wale wa zamani.

Hivyo, hizi hapa ni njia tano ambazo mfanyabiashara yeyote anaweza kutumia kutangaza biashara yake Instagram na kupata wateja zaidi huku akikuza brandi yake:

Matangazo ya ‘sponsored’, baada ya kutengeneza akaunti ya biashara vile inavyopaswa unaweza kuamua ni kiasi gani cha fedha unaweza kutumia kulipia matangazo ya sponsored ambayo yatakuwa yakionekana kwa watumiaji wengine wanaokufuatilia. kikawaida matangazo hayo huwa na chaguzi kadhaa za kulenga hivyo mfanyabiashara anatakiwa kuchagua zile zinazolingana na biashara yake. Akaunti inaweza kutangazwa au chapisho maalum linaweza kutangazwa kuhusu biashara husika, hivyo wakati wa ‘kupromote’ mfanyabiashara ana uhuru wa kuchagua hilo pamoja na aina ya watazamaji katika programu hiyo, rika, jinsia na hata maeneo. Jambo la msingi ni kutengeneza tangazo rahisi linaloelezea kwa urahisi  huduma au  bidhaa kisha kuelezea mawasiliano kwa mfano unaweza kuweka amri inayosema ‘Call now’ au ‘shop now’ nk.

Inaelezwa kuwa matangazo yanayotengenezwa katika ‘insta stories’ huwafikia wafuatiliaji zaidi hivyo mfanyabiashara anaweza kuamua aidha kutangaza katika jukwaa hilo au katika mfumo wa picha kulingana na bajeti yake. Ikiwa mfanyabiashara atatangaza katika ‘insta stories’ ili kuweza kuwahamasisha wateja kuangalia chapisho husika inashauriwa kuweka link katika chapisho husika ambapo mteja ataona maandishi yanayosema ‘see more’ ili tangazo lilete maana zaidi unaweza kuongeza maelezo yanayosema ‘swipe up’ kwaajili ya maelezo zaidi ya huduma au bidhaa husika. kadri wafuatiliaji watakavyokuwa wakijihusisha na machapisho yako ya  ‘insta stories’ watumiaji zaidi wa mtandao huo wataona machapisho yako na aidha kununua, au kuanza kufuatilia biashara yako.

Kuweka bei, wateja wengi hupendelea kuona bei moja kwa moja ili kuweza kufanya maamuzi ya kununua bidhaa au huduma. hivyo ili kuweza kuwahamasisha wateja kupitia instagram kununua bidhaa zako pindi wanapoona machapisho au matangazo yako unaweza kuandika bei aidha katika ‘caption’ au unaweza kuweka ‘tags’ za bei katika machapisho yako. wafanyabiashara wengi wamepoteza wateja kutokana na kuweka mlolongo mrefu unaoelezea bei ya bidhaa au huduma wanazotoa.

Promosheni, hii ni moja ya njia ambayo huongeza wafuatiliaji katika akaunti za biashara instagram. Hivyo mfanyabiashara anaweza kutengeneza utamaduni ambao utawahamasisha wateja kufuatilia akaunti husika. kwamfano mfanyabiashara anaweza kutangaza punguzo la bei kila baada ya muda ili kuweza kumaliza bidhaa za zamani na kuleta bidhaa mpya. Kwa kufanya hivyo wafuatiliaji wapya wataanza kufuatilia akaunti husika ili kuhakikisha hawapitwi na ofa kama hiyo siku zijazo. si lazima iwe ni punguzo la bei mfanyabiashara anaweza kuunda utamaduni  wa kipekee ili kuwahamasisha wafuatiliaji wa zamani na wapya kununua bidhaa au huduma.

Matumizi sahihi ya Hashtags(#), hashtag ni moja ya njia ambazo zinaweza kusababisha chapisho lako katika mtandao wa instagram kuwafikia wafuatiliaji wengi. Hivyo inashauriwa kutumia hashtag chache ambazo zinawalenga wateja unaowalenga. Njia rahisi ya kupata hashtag sahihi ni kuangalia biashara nyingine katika tasnia yako zinatumia zaidi hashtag zipi. Aidha unaweza  kuangalia wahamasishaji ‘influencers’ wengi wanatumia hashtag zipi  ambazo zinaendana na biashara yako kisha tumia ili mradi zitafikisha ujumbe kwa wateja unaowalenga.

Aidha, mitandao ya kijamii imekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara duniani kutokana na urahisi wa kutangaza biashara kulingana na bajeti ikilinganishwa na vyombo vya habari vya kitamaduni kama televisheni, redio na magazeti ambavyo si kila mfanyabiashara anaweza kumudu gharama zake. Hivyo mfanyabiashara anatakiwa kufanya utafiti ili kuweza kujua wateja anaowalenga wanapendelea mitandao ya kijamii ipi ili kuweza kuwafikia kwa urahisi na katika bajeti anayoweza kuimudu ili kuweza kuongeza mapato katika biashara.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter