Uwezo wa watumiaji kufanya utafiti, kulinganisha, na kununua bidhaa na huduma kwa haraka unaonyesha jinsi uaminifu katika bidhaa au huduma fulani umeanza tokea zama za kale. Utafiti uliofanywa karibuni kuhusu watumiaji umeonyesha kuwa asilimia 90 ya watumiaji wanajiona waaminifu katika bidhaa/huduma wanazopendelea.
Jambo hilo si la kushangaza kwa sababu ubora wa bidhaa na huduma ndio mambo muhimu katika utafiti huo. Wateja hawawezi kuendelea kununua bidhaa au huduma katika kampuni inayoendelea kuwagadhabisha kila wakati. Mikataba mizuri na huduma kwa wateja huchangia,
Katika utafiti imeelezwa kuwa asilimia 80 ya wateja hujiona ni waaminifu katika baada ya kununua bidhaa au huduma husika mara tatu tu, na asilimia 37 wamesema inawachukua mara tano kununua bidhaa au huduma ili kujiona ni waaminifu. Wateja hawa ni rahisi kuwa wawakilishi halisi ili mradi kampuni hiyo ikiendelea kutoa huduma nzuri na kujikita kwa wateja wao.
Pia kupitia utafiti huo asilimia 7 ya wateja wamesema huduma kwa wateja ni muhimu. Hata hivyo, ushiriki wa wateja ulikuwa muhimu sana kwa wateja wengi waaminifu. Kwa mfano, asilimia 67 ya wao wanatarajia majibu ya haraka wakati wanatoa maoni. Suala la huduma si tatizo kwa wateja wengi. Wateja wanapendelea zaidi kushirikishwa, kujisikia kama sehemu ya jamii ya biashara hiyo, kwa kufanyiwa mauzo ya kipekee, ni baadhi ya mambo ambayo wateja waaminifu hupendelea.
Huwezi kufanya wateja wawe waaminifu katika biashara/kampuni yako kama hauko makini na vitu muhimu kwao. Kumbuka sheria hizi tatu zinaweza kukusaidia kufanya hivyo:
Kukuza jamii
Ukiweka umakini katika kubadilishwa suala la ushiriki wa wateja katika biashara au hudmua yako, hutakiwi tu kuwasiliana-unatakiwa kuzungumza. Kwa kawaida watu wanapenda mazungumzo hayo mtandaoni, aidha katika mitandao ya kijamii au kwenye vikao vya watu binafsi. Hivyo unda vikao hivyo katika katika jamii na mitandao ya kijamii kuwapa kuwapa wateja wako jukwaa la kujuana na kuwasiliana.
Walete pamoja watu wa rika, washiriki na hata viongozi kwa pamoja ili kufaidisha kampuni yako na zaidi. Jumuhiya utakayounda si lazima izingatie kila unachokitoa katika kampunni yako. Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa brandi yako inatambuliwa na jamii unayoikuza inakua.
Pongeza suala la uaminifu
Kuwahamasisha wateja waaminifu kutasaidia ununuzi endelevu wa bidhaa zako, na kuleta utetezi wa sauti kutoka kwa wateja hao.
Kutoa habari kwa wateja waaminifu kwanza kunawahamasishwa wateja hao ikiwa ni pamoja na kuwapa uwezo wa kununua au kujaribu bidhaa kabla haijawafikia wateja wengine sokoni. Kutoa vitu bure, au katika punguzo la bei na kuwafanya mashabiki wako wakubwa kutokukaa kwenye foleni kutaongeza uaminifu wao na kuwahamasishwa watu wengine kuwa waaminifu ili waweze kupewa kipaumbele pia.
Kubinafsisha mawasiliano yako
Linapokuja suala la kukuza uaminifu wa wateja, utambulisho ni muhimu. Ndio maana leo hii kila kampuni ina mfumo wa kuwasiliana na wateja kwa ukaribu zaidi ingawa si rahisi kufanya hivyo kwa kumaanisha. Hivyo badala ya kutegemea kutuma barua pepe mara moja moja kwa wateja jaribu mbinu zenye nguvu zaidi.
Kwa mfano unaweza kutuma barua pepe kuhusu tabia, kwa mtumia mteja mrejesho kutokana na alivyowasiliana na kampuni yako. Hii itasaidia kuwasiliana na mteja kuhusu jambo ambalo tayari analifikiria kuhusu kampuni yako. Kuwafikia wateja katika siku zao za kuzaliwa, kuathimisha na matukio mbalimbali ni moja ya namna ya kuwafikia wateja wako.
Si lazima uibe benki ili kuweza kufanya haya. Kujipatia uaminifu kwa wateja wako inaweza kuwa rahisi kama ilivyo kwenye ujenzi wa jamii hii ni pamoja na kuongeza ushirikiano, kukua na kusababisha biashara yako au huduma yako iwe ya kuaminika na wateja wanapata uzoefu mzuri na wanaouhitaji. Kwa kufanya hivyo utasaidia biashara au huduma yako kwa namna kubwa sana.