Home BIASHARAUWEKEZAJI Miradi ya Mchuchuma, Liganga kuendelezwa

Miradi ya Mchuchuma, Liganga kuendelezwa

0 comment 135 views

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema Wizara hiyo itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) ili kuhakikisha miradi ya makaa ya mawe Mchuchuma pamoja na mradi wa Chuma Linganga inaanza kutekelezwa.

Nyongo ameeleza hayo wakati akikagua shughuli za madini mkoani Njombe ili kuona namna ambavyo Wizara hiyo inaweza kutatua changamoto zinazohusu utekelezaji wa miradi hiyo. Naibu Waziri huyo amesema kuwa miradi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo inatarajiwa kunufaisha taifa kwa kiasi kikubwa hivyo Wizara ya Madini itashirikiana na wizara hiyo kuhakikisha utekelezaji wake unaanza mara moja.

“Wizara yetu ndiyo inatoa leseni za madini na tayari tulishatoa leseni ya Makaa ya mawe Mchuchuma kwa hiyo nimefika kuangalia changamoto ambazo ziko upande wa Wizara yetu kuweza kuzitatua ili tutoke hapa. Miradi hii tumeisikia miaka mingi ni wakati sasa tunataka ianze”. Amesema Naibu Waziri Nyongo.

Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na Chuma Liganga, inatekelezwa kwa ubia baina ya serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Group Ltd, ya China.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter