Home BIASHARAUWEKEZAJI MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA TMDA WAZINDULIWA

MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA TMDA WAZINDULIWA

0 comment 121 views

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema,Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo  zinapaswa kuwa na mkataba wa huduma kwa  Wateja  ili kurahisisha utoaji wa huduma boara  kwa wanannchi.Hayo ameyasema  Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi jijini Dar es Salaam wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), amesema kuwa TMDA imekuwa na mipango mizuri katika utoaji wa  huduma kwa kuzingatia muda katika utoaji wa leseni kwa wadau mbalimbali.

Profesa Makubi amesema kuwa TMDA imekuwa na mifumo ya viwango ambapo Shirika la Afya Duniani inatambua pamoja na jumuiya  mbalimbali na hiyo inatokana na mikakati ya watendaji wa taasisi waliojiwekea ya kuhakikisha wanakwenda kutatua matatizo ya  huduma katika utoaji wa huduma.

Amesema  kuwa TMDA inatoa mkataba  mara ya nne ambapo amewataka mamlaka hiyo  kufuatilia mkataba huo kuona malengo waliojiwekea yameweza kama wameweza waliojipangia pamoja na huduma wanazozitoa kwa wadau.

Nae Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema kuwa katika mkataba huo wamezingatia muda wa utoaji wa usajili  za waingizaji dawa kutoka siku 240 hadi 180 na wa ndani kutoka siku 120 hadi siku 60 na usajili dawa sehemu za biashara kutoka siku 10 hadi 8.Fimbo amesema kuwa mkataba huo umezinagatia  maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma  na kuleta ufanisi pamoja na kuweka mikakati kuendelea kutoa huduma  bora
kwa wadau amesema  TMDA  tangu walipoanza kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja wamekuwa na mafanikio  makubwa  katika utoaji wa huduma bora kutokana na watendaji kujipanga katika kuhudumia wateja hao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter