Home BIASHARAUWEKEZAJI Ndege 4 kuwasili ifikapo 2024

Ndege 4 kuwasili ifikapo 2024

0 comment 66 views

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema ndege nne zinatarajiwa kuwasili nchini ifikapo Februari, 2024.

Prof Mbarawa amesema hayo wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ya Wizara hiyo.

“Miongoni mwa maeneo muhimu ambayo Serikali imeendelea kutekeleza katika uimarishaji wa ATCL ni pamoja na kuendelea na usimamizi wa utengenezaji wa ndege mpya nne ambazo zitasaidia kuiongezea ATCL kupanua mtandao wa safari za ndani na nje ya Nchi ili kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchumi kama utalii, biashara, kilimo, mifugo, uvuvi, na kadhalika.

Ndege mpya zilizonunuliwa ni Boeing 767-300F moja ya mizigo inayotarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi Mei, 2023, Boeing 737-9 mbili zinazotarajiwa kuwasili mwezi Agosti na Disemba, 2023 na Boeing 787-8 Dreamliner ndege moja (1) inayotarajiwa kuwasili mwezi Februari, 2024, Waziri Prof Mbarawa ameeleza bungeni Dodoma.”

Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 ATCL kwa kutumia ndege 11 ilizonazo imeendelea kutoa huduma ya usafiri wa anga ndani na nje ya nchi, jumla ya vituo ambavyo ATCL imetoa huduma ni 24 ambapo vituo 14 ni vya ndani ya nchi na vituo 10 ni vya nje ya nchi.

Amevitaja vituo vya ndani ya nchi kuwa ni Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Songwe, Geita, Tabora, Kilimanjaro, Kigoma, Mpanda, Mtwara, Mwanza, Songea, na Zanzibar na vituo vya nje ni Bujumbura, Nairobi, Entebbe, Hahaya, Guangzhou, Harare, Lubumbashi, Lusaka, Ndola na Mumbai.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter