Home BIASHARAUWEKEZAJI Rwanda kuongeza uwekezaji Tanzania

Rwanda kuongeza uwekezaji Tanzania

0 comment 101 views

Maofisa wakuu wa Rwanda, akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Soraya Hakuziyaremye, Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Richard Sezibera, na Waziri wa Miundombinu, Balozi Claver Gatete wamefanya ziara katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania mkoani Kagera (kwa upande wa Tanzania) ili kujua changamoto zilizopo. Nchi hiyo ina mpango wa kuongeza huduma mpakani ili kuhudumia idadi kubwa ya mizigo ambayo hupita mpakani hapo.

Imeelezwa kuwa mpaka huo hupitisha asilimia 95 ya bidhaa zinazoingia katika nchi hiyo zikitokea bandari ya Dar es Salaam na magari ya mizigo takribani 270 huingia kila siku. Kutokana na idadi ndogo ya wafanyakazi, taratibu za uhakiki wa mizigo zimekuwa tatizo.

Pamoja na hayo, Rwanda ina matarajio ya kujenga soko la kisasa katika mpaka huo ili kuimarisha biashara. Waziri wa Viwanda na Biashara wa nchi hiyo, ametaja baadhi ya changamoto walizogundua wakati wa ziara hiyo kuwa ni ukosefu wa miundombinu mpakani, ucheleweshaji wa ukaguzi wa malori yanayobeba mizigo pamoja na uwepo wa wafanyakazi wachache.

“Mpaka huu ni moja ya mipaka muhimu kwetu, hivyo ziara hii itatuwezesha kuboresha mtiririko wa biashara mpakani kati ya Rwanda na Tanzania. Tutachukua hatua na kufanya maamuzi  jinsi ya kuongeza watumishi na jinsi ya kupanua miundombinu katika mpaka huu”. Amesema Waziri Hakuziyaremye.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter