Home BIASHARAUWEKEZAJI SERIKALI KUONGEZA MAABARA ZA MIFUGO

SERIKALI KUONGEZA MAABARA ZA MIFUGO

0 comment 64 views

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa maabara za mifugo kwenye kila mkoa.

Pia amesema udahili wa wanafunzi wa ngazi ya astashahada na shaahada katika fani mbalimbali za afya ya mifugo imeongezeka kwa asilimia 43.3.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Singida Kaskazini, Justine Monko (CCM) aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuongeza wataalam ama vitendea kazi kama njia mbadala ya kuwasaidia wataalamu wachache waliopo kutoa huduma bora kwa wafugaji.

Pia alitaka kujua ni lini Serikali itajenga maabara za mifugo katika maeneo ya wafugaji ili wananchi waache kutibu mifugo yao kwa kubahatisha. Akijibu swali hilo, Mpina alisema Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa maabara za mifugo kwenye kila mkoa. Alisema mpaka sasa kuna maabara za mifugo za Serikali kumi na moja kwenye kila Kanda.

“Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara inategemea kujenga Kliniki za mifugo zenye maabara katika halmashauri mbili za Chato na Meatu. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara imepanga kujenga Kliniki zingine 10 kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Sindiga Vijijini.

Mpina alisema Wizara pia imeshavielekeza vituo binafsi 1,709 vya kutolea huduma ya afya ya mifugo vilivyopo kwenye Halmashauri zote 185 kuhakikisha vinakuwa na maabara ndogo kwa ajili ya kutoa huduma ya uchunguzi wa awali wa magonjwa ya mifugo.

Aidha, Mpina alisema katika kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la maafisa ugani wa mifugo, Serikali imejikita kuongeza udahili wa wanafunzi wa ngazi ya astashahada na stashahada wa fani mbalimbali afya ya mifugo kwa asilimia 43.3.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter