Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali ya Tanzania yatangaza fursa uwekezaji viwanda 20

Serikali ya Tanzania yatangaza fursa uwekezaji viwanda 20

0 comments 505 views

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Tanzania, Kitika Mkumbo amesema Tanzania ina jumla ya viwanda 80,969 ambapo kwa sasa viwanda 20 vinatafutiwa wawekezaji.

Viwanda hivo ambavyo vimegawanywa katika makundi manne, ni viwanda vidogo sana, viwanda vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma Agosti 23, 2021 waziri Mkumbo amesema “Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wamekalimisha utafiti wa awali wa kutathimini maendeleo ya sekta viwanda kwa sasa ambapo ukijumlisha makundi tuna viwanda 80,969 mpaka Julai, na hii ni taarifa amabayo tumeipata juzi tumeifanya sisi na wenzetu wa NBS, ni survey kubwa”.

Katika viwanda hivo, viwanda vidogo sana vipo 60,463, viwanda vidogo 17,267, viwanda vya kati 684 na vikubwa 618.

Amefafanua kuwa viwanda vidogo sana ni vile vinavyoajiri kati ya mtu mmoja mpaka wanne na mtaji wake hauzidi milioni tano.

Viwanda vidogo ni vile vinavyoajiri watu watano mpaka 49 na mtaji wa kati ya milioni tano mpaka milioni 200, kiwanda cha kati kikiwa na uwezo wa kuajiri watu 50 mpaka 99 na mtaji wa milioni 200 hadi mia 800 huku kiwanda kikubwa kikiwa na watu 100 na zaidi na mtaji wa zaidi ya milioni 800.

“Kwa sasa viwanda vikubwa nchi nzima tunavyo 618 na katika hivo viwanda 208 vipo Dar es Salaam, karibu theluthi ya viwanda vyote vikubwa vinapatikana jijini Dar es Salaam” amesema Waziri Mkumbo.

Aidha, waziri Mkumbo ameongelea viwanda vilivyo binafsishwa ambapo amesema kama sehemu ya kutekeleza sera ya kuimarisha sekta binafsi na kuipa nafasi sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya uchumi kikamilifu miaka ya tisini serikali ilibinafsisha viwanda na mashirika mbalimbali ya umma ambapo kwa upande wa viwanda serikali ilibinafsisha viwanda 156.

2017 serikali iliamua kufanya tathimini ya kina kuhusu maendeleo ya viwanda vyote amabavyo vilibinafsishwa kwa kuangalia mikataba ambayo ilikuwepo ni kiasi gani imetekelezwa.

Viwanda vyote 156 vilifanyiwa tathimini, na tathimini ilionesha kwamba viwanda 88 vilikuwa vinafanya kazi vizuri na vinafanya kazi kwa kiasi kikubwa iliyokusudiwa kwa mujibu wa mikataba ya serikali na wawekezaji.

Viwanda 68 vilikuwa havifanyi kazi vizuri ambapo kati ya hivo viwanda 20 vilishapoteza sifa ya kuwa viwanda.

“Wawekezaji wa viwanda hivi hawakuzingatia masharti na matakwa ya mikataba, timu ya serikali ikaingia kwenye majadiliano na wawekezaji hawa kwa lengo la kurudisha viwanda hivi serikalini kisheria, katika viwanda 48 tayari serikali imesharudisha viwanda 20”.

Amesema kwa mujibu wa sera ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa inaipa sekta binafsi nafasi ya kuendesha uchumi ambapo serikali inashirikiana nao kwa ubia kati ya sekta binafsi na serikali.

“Tunaenda kuwakaribisha na kuwaita na kuwaomba wawezekaji wa sekta binafsi wajitokeze kuwekeza katika viwanda hivi 20”.

Ameeleza kuwa viwanda 10 vinatafutiwa wawekezaji wapya kutoka sekta binafsi kwa ajili ya kuviendeleza, viwanda nane vimekabithiwa kwa Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) kwa ajili ya uwekezaji kwenye maeneo ya uzalishaji wa kiuchumi ambapo EPZA itaandaa utaratibu wa kupata wawekezaji katika maeneo hayo.

Viwanda viwili vitakabidhiwa kwa mashirika ya umma ili waviendeleze kwa kuingia ubia na wawekezaji wa sekta binafsi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!