Home BIASHARAUWEKEZAJI Tanzania kuendelea kushirikiana na China

Tanzania kuendelea kushirikiana na China

0 comment 100 views

Shirika la Bima la China – (CHINA EXPORT AND CREDIT INSURANCE CORPORATION (SINOSURE), imeahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na Tanzania ambao umekuwepo kwa muda mrefu kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo ya watu.
Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Zha Weimin alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Weimin amesema SINOSURE inafanya juhudi kuwezesha ushirikiano kati ya Tanzania na China kuwa wenye matokeo chanya kwa kushawishi kampuni nyingi za China kuwekeza katika miradi mbalimbali na kufanya biashara Tanzania.
Kwa Upande wake Waziri Dkt. Nchemba amewahikikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kujizatiti kufanya kazi na kushirikiana na Serikali ya China ili kuboresha ushirikiano wa nchi hizo mbili ambao umekuwepo kwa muda mrefu ili kuleta maendeleo ya wananchi.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa msaada mkubwa kwa sekta mbalimbali za uchumi wetu ikijumuisha Miundombinu ya Reli, Elimu, TEHAMA, Nishati, Maji, Usalama, Viwanda na Sekta za Afya.

Ni matumaini yetu kuwa ushirikiano huu wa pamoja utaendelea kuimarika zaidi” amesema Dkt. Nchemba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter