Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji wa China wakamatwa Morogoro

Wawekezaji wa China wakamatwa Morogoro

0 comment 105 views
Na Mwandishi wetu

Siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza uongozi mkoani Morogoro kufuatilia kampuni ya Zhong Feng, raia watatu wa China wamekamatwa na vyombo vya ulinzi vya mkoa huo kwa madai ya kuendesha shughuli za uwekezaji bila kufuata taratibu za kisheria za hapa nchini.

Akizungumzia juu ya suala hilo, Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe amesema agizo la kuwa kamata raia hao limekuja mara baada ya kugundulika kuwa wanajihusisha na uchimbaji wa madini yanayotengeneza marumaru bila kufuata kanuni na sheria za nchi.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Omary Mgumba, wawekezaji hao wamekuwa wakiendesha shughuli hizo jimboni kwake bila kibali tangu mwaka 2011. Ameongeza kuwa serikali imekuwa ikikosa mapato kwani watu hao wamekuwa wakikwepa kulipa kodi za serikali pamoja na tozo mbalimbali za halmashauri.

Hivi sasa wawekezaji hao wapo chini ya ulinzi huku wakisubiri taratibu za kuwarudisha nchini kwao zikamilike. Dk. Kebwe ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha raia hao wanafikishwa jijini Dar es salaam na kusafirishwa hadi kwao haraka iwezekanavyo. Wakati yote hayo yakiendelea, mali za mgodi huo zimewekwa chini ya uangalizi wa jeshi la polisi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter