Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za kisasa maarufu kama smartphone, suala la kufanya biashara kupitia mitandao nalo limeendelea kushika kasi. Imekuwa rahisi kutafuta wateja na kuuza bidhaa pia imekuwa rahisi kutafuta wanunuzi na kuuza aidha vitu vipya au vilivyo tumika kwa kutumia mitandao na applications za simu mbalimbali.
Hizi hapa ni baadhi ya application ambazo unaweza kutumia kufanya biashara kwa urahisi
eBay
Hii application inawaunganisha wafanyabiashara na wanunuzi wa dunia nzima hivyo ni rahisi kuuza au kununua bidhaa za ndani na hata nje ya nchi. Unachotakiwa kuzingatia ni thamani ya bidhaa yako na uwezekano wa kutuma bidhaa hiyo kwenda sehemu mbalimbali. Pia ni muhimu kuweka taarifa zote kuhusu bidhaa hiyo ili awe na taarifa zote muhimu kabla ya kununua.
Hii humruhusu mtumiaji kutuma picha au video katika akaunti yake na watu wanaomfuatilia (follow) wanaweza kuona. Hivyo kama una bidhaa unauza ni rahisi kupiga picha na kuweka Instagram kwa ajili ya kujipatia wateja pia kama unahitaji bidhaa fulani ni rahisi kuipata katika mtandao huu kwa sababu wafanyabiashara wengi hivi sasa wanatumia sana mitandao ya kijamii. Kama unanunua katika mtandao huu unashauriwa kuwa makini kwa sababu sio kila muuzaji ni muaminifu hivyo unashauriwa kulipia pale utakapopata bidhaa husika. Kwa upande wa wafanyabiashara, ni muhimu kuwa muaminifu kwa sababu kumekuwa na tabia ya kutumia picha nzuri mtandaoni na kumpelekea mteja bidhaa tofauti na iliyokuwepo katika picha. Kama una mpango wa kukuza biashara yako kuwa muaminifu, weka bei zinazoendana na bidhaa unazouza.
Amazon
Hii application ilianzishwa kwa nia ya kuuza vitabu kwenyemtandao, lakini hivi sasa watumiaji wake wana uwezo wa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Amazon inasifiwa kwa kuwa na mfumo mzuri kwa ujumla kama kwenye masuala ya kupeleka bidhaa kwa mteja. Mtandao huu pia unamruhusu mteja kurudisha bidhaa kama hajaridhika nayo. Application hii ina bidhaa aina nyingi hivyo kumrahisishia mteja kuchagua na kujenga ushindani baina ya wafanyabiashara. Ni muhimu kwa mfanyabiashara kujua kama anauza bidhaa katika mtandao huu kwa kujifurahisha au kama ajira, kwa sababu Amazon huwafuta wafanyabiashara ambao hawana ushindani mkubwa.
Hivi sasa mtumiaji amepewa uhuru wa kutumia Facebook bure. Kuna makundi mengi sana yanayohusu biashara hivyo mfanyabiashara ana uwezo wa kuchagua kundi linalofaa bidhaa zake kwani watumiaji huenda katika makundi husika kupata bidhaa anayotaka.
Taobao
Hii ni application ya China ambayo watanzania wengi hutumia. Ipo chini ya kampuni ya Alibaba Group. Kuna bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu ambazo mteja anaweza kununua. Kama mteja akiagiza bidhaa kutoka China kuja nchini muda hutofautiana kulingana na njia ya usafiri. Kwa mfano ukiagiza kupitia DHL, basi bidhaa itafika baada ya siku 5 hadi kumi, EMS siku 10 hadi 28 n.k. Ikiwa unataka bidhaa ifike haraka zaidi basi itabidi ulipie fedha zaidi kuharakisha usafirishaji.