Home BIASHARA Vodacom Tanzania yazindua duka Aura Mall

Vodacom Tanzania yazindua duka Aura Mall

0 comment 130 views

Kampuni ya simu za mkononi Vodacom, imezidi kusambaza huduma  karibu na wateja wake kwa kufungua ‘vodashop’ katika jengo la Aura Mall jijini Dar es Salaam. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar na Pwani, George Lugata pamoja na wafanyakazi wengine wa Vodacom.

 

Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar na Pwani, George Lugata (kushoto) na bwana Mirza Ngoshani (mwenye Tshirt ya blue) wakikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom katika jengo la Aura mall hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa, kampuni ya Vodacom ina maduka 100 na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya litakalotoa huduma kila siku kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku.

Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Kanda ya Dar na Pwani, George Lugata (wa pili kulia) akizungumza na wageni na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika jengo la Aura mall jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom ina maduka 100 na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya litakalotoa huduma kila siku kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter