Na Mwandishi wetu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof. Faustine Bee amesema vyama vya ushirika vina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wakati huu ambapo serikali inahamasisha mchakato wa Tanzania ya viwanda.
Ameyasema hayo akiwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye majadiliano mafupi yenye nia ya kubadilisha mtazamo wa jinsi watu wanavyochukulia vyama vya ushirika. Ameongezea kwamba mfumo huu ni mzuri kwa kukuza uchumi hapa nchini.
Ushirika ndiyo njia pekee ya kujenga uchumi utakaomilikiwa na watanzania. Prof. Faustine amesisitiza kuwa ushirika utajenga uchumi ambao utamuondoa mtanzania katika umasikini na kufanya aweze kumiliki rasilimali za nchi. Utapeli unaofanywa na watu wachache ndio unapelekea vyama hivyo kuonekana kama kitu kibaya katika jamii.
Naibu Mkuu wa chuo hicho, Goodluck Mmari naye amesema ushirika ndiyo njia pekee ya kumkomboa mtu mwenye kipato kidogo sio tu hapa nchini bali duniani kote.