Home BIASHARA Wafanyabiashara wakumbushwa kutunza taarifa

Wafanyabiashara wakumbushwa kutunza taarifa

0 comment 98 views

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Singida, Watson Mmasa ametoa wito kwa wafanyabiashara mkoani humo kuwa na mazoea ya kutunza taarifa za biashara zao na pale zinapohitajika, kuzitoa kwa umakini kwa ajili ya ukadiriaji kodi na ukaguzi. Mmasa amesema hayo wakati wa semina ya elimu kwa mlipakodi na kuongeza kuwa, taarifa hizo zinaondoa usumbufu na kurahisisha zoezi zima la ukadiriaji kodi.

“Nawasihi wafanyabiashara wa mkoa wa Singida, mtunze taarifa za kibiashara kwa usahihi ili tunapokuja kukagua tupate taarifa sahihi za kutuwezesha kukukadiria kwa usahihi, sawasawa na biashara unayoifanya, lengo letu sio kukandamiza bali ni kutenda haki”. Amesema Kaimu huyo.

Aidha, Ofisa Elimu kwa mlipakodi mkoani humo, Zacharia Gwagilo amewataka wafanyabiashara kuwasilisha ritani za kodi kwa wakati unaotakiwa na kwa mujibu wa tarehe zilizoainishwa kwenye kalenda ya ulipaji kodi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) mkoa wa Singida, Florian Malya ameishukuru mamlaka hiyo kwa semina hiyo akisema itachangia kwa kiasi kikubwa uelewa wa masuala ya ulipaji kodi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter