Wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wilayani Kahama wameandamana wakidai kulipwa sitahiki zao baada ya kuondolewa kazini. Wafanyakazi hao wameonekana katika mitaa kadhaa ya mji huo wakielekea ofisi za NSSF wakitaka kulipwa mafao yao ambayo wamedai ni ya muda mrefu.
Wafanyakazi hao wamedai kabla ya kuondolea kazini, walielezwa mafao yao yapo tayari lakini wamekuwa wakienda katika ofisi za NSSF mara kwa mara na kutopatiwa fedha zao huku watumishi wa shirika hilo wakiwaeleza kuwa wangezitumia fedha zao vibaya.
Akizungumzia sakata hilo, Meneja wa NSSF mkoa maalum wa Kahama Wiston Mdingile amesema wameshindwa kuwapatia wafanyakazi hao fedha zao kwa sababu kampuni ya Acacia imepunguza watumishi wengi kwa wakati mmoja hali ambayo imepelekea madai mengi kufunguliwa kwa pamoja hivyo shirika hilo kushindwa kulipa watu wote kwa wakati. Amewataka wafanyakazi hao kuwa wavumilivu kwani NSSF imekuwa ikiwalipa wote wanaodai mafao yao kwa awamu.