Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara kwenye makao makuu ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es Salaam na kujionea utendaji kazi wa kampuni hiyo kwenye mfumo wa kidijitali. Mhandisi Nditiye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dr. Jim Yonaz pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akisikiliza kuhusu utendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Hisham Hendi (wa pili kulia) alipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom mapema leo na kujionea namna ambavyo kampuni hiyo inafanya kazi zake kidijitali. Kushoto ni Naibu Katibu mkuu wa Wizara hiyo, Dr Jim Yonaz na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Mhandisi Peter Ulanga.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (wa kwanza kushoto) wakisikiliza shughuli zinazofanywa na kitengo cha Ufanisi wa mtandao kutoka kwa Mhandisi Pendo Boshe wa kitengo hicho wakati wa ziara ya naibu waziri katika ofisi za Vodacom Tanzania mapema leo, ambapo naibu waziri alijionea namna ambavyo kampuni hiyo inafanya kazi zake kidijitali.