Home Elimu CORONA: Fahamu hatua salama za kutumia mask.

CORONA: Fahamu hatua salama za kutumia mask.

0 comment 106 views

Kumbuka, mask inapaswa kutumiwa tu na wafanyikazi wa afya, watoa huduma, na watu wenye dalili za corona, dalili kama shida ya kupumua, homa na kikohozi.

Fuata taratibu hizi ili kuweza kutumia mask kwa usalama zaidi.

  1. Kabla ya kugusa mask, hakikisha mikono yako ni misafi kwa kunawa maji na sabuni au kwa kutumia kitakasa mikono (sanitizer)
  2. Chukua mask na ikague kama haijatoboka au kuchanika.
  3. Ikague tena kujua upande upi ni wa juu upi ni wachini. (upande wa juu ni ule wenye kiwaya).
  4. Hakikisha upande mzuri wa mask ni upi, upande wenye rangi uwe nje.
  5. Weka mask kwenye uso wako. Weka vizuri sehem ya juu yenye kiwaya na sawazisha vizuri mask yako kutengeneza sura ya pua yako.
  6. Fungua upande wa chini ya mask ili kufunika mdomo wako na kidevu chako.
  7. Baada ya matumizi, ondoa mask; anza kwa kuvuta mpira kutoka nyuma ya masikio, epuka kugusa upande wa mbele wa mask.
  8. Tupa mask hiyo kwenye pipa la taka lililofungwa mara baada ya matumizi.
  9. Fanya usafi wa mikono baada ya kugusa au kutupa mask – Tumia maji na sabuni au kitakasa mikono (sanitizer) kusafisha mikono yako baada ya kutupa mask.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter