Home Elimu Kuna uwezekano nusu ya ajira kutoweka 2050

Kuna uwezekano nusu ya ajira kutoweka 2050

0 comment 133 views

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam na kuelezea utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

“Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa,” amesema  Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

“Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva” amesema naa kuongeza kuwa kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii.

Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu katika sayansi na teknolojia ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

“Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter