Unatakiwa ukubali udhaifu wako lakini kusanya nguvu kupitia hayo na ujifunze kitu ndani yake.Unapofanya kosa chukua nafasi ya kutafuta nafasi ya pili kusahihisha kosa hilo na ukusanye uzoefu mpya.
3.WEWE NDIO WA KWANZA KUKUTANA NA MAGUMU?
Maisha huanza na maisha huisha,kuna muda maisha yanacheka na maisha yanalia,maisha yanakata tamaa na maisha yanajaribu.
Maisha yana picha tofauti katika macho ya kila binadamu aliye juu ya ardhi.Ukweli ni kuwa vile ulivyokuwa zamani,ulivyo sasa na yule utakayekuja kuwa ni watu watatu tofauti.
4.MAUMIVU YAMEKUSAIDIA NINI?
Kuna muda lazima mambo yabadilike ili na wewe ubadilike.Lazima kuna muda upate maumivu ili ukue kiuzoefu.
Kuumia ni lazima ili upate hekima ambayo haukuwahi kuiwaza kama utaipata.Lazima uumie moyo ili uanze kuufuata moyo wako katika maamuzi sahihi.
5.KUFANIKIWA NI KUWA NA NINI?
Usiruhusu mahangaiko yako ndio yakutambulishe kwa watu wewe ni nani.Sio kila kitu unavyokitarajia kiwe kitakuwa hivyo hivyo ulivyodhani wewe.Na ndio maana unapaswa kuacha kuishi matarajio,ishi wakati ulionao na fuata mkondo na si kwenda kinyume na njia ya mkondo.Jikumbushe kuwa ni ukamilifu kutokuwa mkamilifu.Mafanikio si kitu unachopata,ila ni uwezo wako wa kufanyia kazi uliyojifunza na kuyatumia kwa ufanisi katika uhalisia wa maisha yako.
6.KUNA NJIA NYINGINE YOYOTE?
Tofauti ya njia nyembamba na ndogo inajengwa na mtazamo wako.
Na hapo ndio unapaswa ujue kuwa ili kubadilisha kitu ni lazima ubadilishe mtazamo wako.Kutoweza kuona njia mbadala katika maisha yako inatokana na mtazamo wako kujifungia eneo moja la maisha.
7.KUNA JAMBO LINAWEZA KUFANIKIWA BILA KIKWAZO?
Hata kama haupo sehemu ambayo ulitamani kuwa haimaanishi kuwa hautakuwa siku moja.
Kufanikiwa kunaambatana na kujitambua ambapo kutakusaidia kupambana mpaka mwisho.
Mafanikio bila ya vikwazo vitakufanya usione thamani yake na unaweza kuyatumia vibaya.Ukuta uliokutenga na ndoto yako unakusaidia kufahamu ni jinsi gani utajitoa kufikia unalotamani kwa kuuvunja.
8.ZURI NI HILO TU?
Unaweza ukawa umekutana na mabaya wakati unatafuta mazuri fulani,lakini haimaanishi hayo mazuri uliyoyakosa ndio pekee yaliyopo duniani.Maisha yana mambo mengi mazuri na si yale tunayodhani sisi kuwa ni mazuri na kuyaona mengine kuwa mabaya kwa kuwa ndivyo tunavyodhani.
KUKATA TAMAA KATIKA MAISHA, SI KITU CHA KUKIFIKIRIA KWANZA PALE UNAPOKUMBANA NA MAGUMU.
HAKUNA UTAKALOPANGA KULIPATA,UKALIPATA KIRAHISI RAHISI KAMA WENGI WETU TUNAVYOTAMANI IWE.
TUMIA MASWALI HAYO HAPO JUU,KUJIULIZA PALE UNAPOKUMBANA NA WAKATI MGUMU ILI USIKATE TAMAA.