Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bandari cha Dar es Salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa kuna fursa za kutosha kwenye chuo hicho vijana wazichangamkie ili wapate ujuzi na kuingia kwenye soko la ajira.
Dkt. Gurumo ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Akizungumzia maendeleo ya chuo hicho amesema kimeongeza udahili kutoka wanafunzi 5,563 wa mwaka 2013/2014 hadi 9,034 kwa mwaka 2021/2022.
Ámeeleza kuwa udahili huo umeongezeka kutokana na serikali kutoa kipaumbele kwa matumizi ya vyanzo vya maji kwa maendeleo ya kiuchumi,.
Amesema “tunatarajia kuwa na wanafunzi zaidi ya 20,000 ifikapo mwaka 2025/2026.”
Amefafanua kuwa katika mwaka wa masomo 2022/2023 DMI imedahili wanafunzi wa ngazi ya Shahada ya Pili katika jumla ya kozi tano za International Trade and Maritime Law, Shipping and Logistics Economics; Maritime Transport and Nautical Science; Marine Engineering Management na Transport and Supply Chain Management.
“Kumekuwa na ongezeko la mikopo ya wanafunzi ambapo mwaka 2021/2022 wanafunzi zaidi ya 850 walipata mkopo kulinganisha na wanafunzi 1705 walipata mkopo kwa mwaka 2022/2023.
Áidha, zaidi ya nusu ya wanafunzi waliopata mkopo wamepata kwa asilimia 100.
Amesema Chuo kinafanya tafiti na kutoa ushauri elekezi kwa serikali na taasisi binafsi.
Baadhi ya shughuli zinazofanywa ni usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri majini, ‘stability testing’, ‘inclination and tonnage testing’ na tathimini ya njia za vyombo vya majini katika vyanzo vya maji.