Home Elimu Watunzi wa filamu wanolewa

Watunzi wa filamu wanolewa

0 comment 135 views

Takriban watunzi 37 wa filamu kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamepata mafunzo kwa lengo la kuinuka na kukuza sanaa ya filamu.

Mafunzo hayo yamefanyika katika hoteli ya Serena mjini Unguja yameandaliwa na Multichoice Talent Factory kwa kushirikiana na Zanzibar International Film Festival (ZIFF).

Akizungunza na waandishi wa habari Mkurungenzi wa Multichoice Africa Nwabisa Matyunza amesema kwa uapande wa Zanzibar, sanaa bado ipo chini kutokana na ukosefu wa elimu ya kitaalumu hasa kwa watunzi jambo linalopelekea kushuka kwa sanaa visiwani humo.

Aidha ameongeza kuwa matarajio yao baada ya mafunzo hayo wasanii watafanya kazi zenye ubora na kufika viwango vya kimataifa.
Mkurungenzi wa ZIFF Martin Muhando ameishukuru Multichoice kwa ushirikiano wao wa kukuza vipaji vya wasanii na kuhakikisha wanafika viwango vya juu.

Nae Katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Kiagho Kilonzo amesema serikali itaendelea kushirikiana na watasisi mbalimbali zenye kuboresha sanaa ambayo itatoa ajira nzuri kwa vijana na kuleta tija kwa taifa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Africa Multichoice Talent Factory Kwa kushirikiana na ZIFF pamoja na bodi ya filamu Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter