Home FEDHA Agizo la Biteko kwa Bodi STAMICO

Agizo la Biteko kwa Bodi STAMICO

0 comment 117 views

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha kuwa, sekta hiyo inaongeza mchango wake katika pato la taifa, kwa kulipa kodi mbalimbali za serikali, kupanua wigo wa ajira kwa wananchi na vilevile, kwa kulipa mrahaba.

Biteko amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo jijini Dar es salaam na katika maelezo yake ameongeza kuwa, anatambua umuhimu mkubwa wa Bodi hiyo pamoja na mchango wake katika kufanya maamuzi, kupitia Sheria na sera za uendeshaji wa shirika hilo kwa ujumla.

Waziri huyo pia ametumia fursa hiyo kupongeza Shirika hilo kwa kutekeleza baadhi ya miradi ikiwa ni pamoja na uchimbwaji na uuzwaji wa makaa ya mawe Kabulo, uchenjuaji wa mabaki ya mchanga wa dhahabu katika eneo la mradi wa dhahabu wa Buhemba, kuzalisha na kuuza kokoto Ubena Zomozi, kuimarisha usimamizi wa miradi ya ubia ya Tanzanite One na Buckreef na kampuni tanzu ya STAMIGOLD, na vilevile kuratibu shughuli za kuwaendeleza wachimbaji wadogo.

Mbali na Waziri Biteko, uzinduzi wa Bodi hiyo pia ulishirikisha viongozi waandamizi wa Wizara ya Madini ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri, Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter