Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Biashara unayoweza kuifanya ukiwa mwanachuo

Biashara unayoweza kuifanya ukiwa mwanachuo

0 comment 252 views

Je wewe ni mwanachuo na ungependa kufanya biashara wakati unasoma?Basi kama jibu ni ndiyo na baada ya kuona unaweza kupata muda wa kutosha kufanya biashara bila ya kuharibu ratiba zako za masomo,swali litakalokua la msingi ni je ufanye biashara gani?

Kuna biashara nyingi unazoweza kufanya kutokana na kile ama kulingana na kile unachopenda wewe na hata vipaji ulivyonavyo.Ila ningependa tushirikishane baadhi ya biashara ambazo mwanafunzi anaweza kufanya kwa muda huo utakaokua wa ziada kwake.

Ujasiliamali wa taarifa.

Hii ni biashara ya kutoa taharifa mbalimbali zinazoweza kusaidia mtu mmoja mmoja ama jamii kwa ujumla zinazoweza kuwasaidia watu na hatimaye wakawa na utayari wa kukulipa kutokana na taharifa utoazo.Kuanza biashara hii unachakua ni aina gani ya tahaarifa ambazo unapenda kufatilia au kutoa kasha ukaanzisha blogu ambayo utaitumia kutoa taharifa hizo,taharifa zinaweza kua za kuelimisha,kuburudisha,ajira kwa wajasiliamali na hata kutoa hofu na mawazo potofu katika jamii na ukafaidika kwa njia hiyo.Ukitoa taharifa nzuri na za ukweli utapata wafatiliaji wengi na hata ikakupa uwezo wa kuwauzia bidhaa adhira yako au kuuza nafasi za matangazo kwenye blogu yako hiyo na ikakuingizia kipato kizuri.

Biashara ya mtandao.

Hii ni biashara ambayo inaweza kufanyika katika muda mchache kila siku na kila wiki na baada ya mwaka moja ikakulipa kiasi kizuri cha pesa na hata kukupatia mafanikio makubwa.

Hii ni biashara ambayo unatengeneza mtandao ama jukwaa la wa watumiaji wa huduma ama bidhaa fulani na hivyo watu wanatumia mtandao/jukwaa lako kutangaza biashara zao ama huduma zitolewazo na wao na hivyo wateja wao wanapotumia huduma yao ama kununua bidhaa kupitia mtandao wako unapata kamisheni.

Makampuni mengi sana kwa sasa yanafanya biashara hii kwa hapa kwetu Tanzania,na kama tu utazifatilia kwa makini utakuta unatengeneza pesa kupitia njia moja wapo rahisi ambayo aitoingiliana na muda wa masomo yako.

Tumia vipaji vyako.

Kila binadamu,Mungu alimpatia uwezo wa kufanya mambo zaidi ya mwingine,hii inamaanisha kila binadamu ameumbwa na kipaji chake ama kitu anachopendelea kufanya zaidi.Hivyo basi unaweza kutumia muda huu wa chuo kuendeleza kipaji/vipaji vyako kuangalia ni kipaji gani kinaweza kufanya ukaingiza pesa na watu wakakulipa kupitia kipaji chako,unaweza kua na kipaji cha kuchora,mitindo,mchezo wa mpira,kuimba,kuandika.Tenga muda maalumu wa kuendeleza kipaji chako kila siku,kwa mfano wewe ni muimbaji na unapenda kuimba,jaribu kutenga muda wa saa 1 kufanya mazoezi ya kuimba ili t uboreshe uimbaji wako.

Biashara ya uchuuzi wa kawaida.

Kama kuna nafasi kubwa ya wewe kuweza kutumia muda wako utakao kua free,basi utumie katika kufanya biashara ndogo ndogo kwa maeneo ya chuoni au unakoishi.Angalia katika eneo lako la chuo ama unapoishi ni bidhaa gani,ama ni huduma gani wanafunzi wanazihitaji ila wanazikosa au hawazipati kwa kiwango kizuri kisha ingia kwenye biashara hiyo.Kama uta bahatika kufanya hivyo basi jitahidi kutoa huduma nzuri sana,au tofauti na watu wanaofanya biashara kama yako.Utaona faida baada ya kua umefatilia hayo.

Biashara ya teknolojia.

Teknolojia ni sekta inayokua kwa kasi sana.Basi kama uko chuo na ni mtumiaji wa kompyuta au mtandao unaweza kujiingizia kipato kwa kutumia kompyuta yako kama kutengeneza Blogu,kutengeneza tovuti pia hata kuweka ubunifu katika picha ili tu kompyuta yako iwe moja kati ya chanzo chako cha mapato.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter