Home FEDHABIMA Mambo ya kuzingatia unapochagua bima

Mambo ya kuzingatia unapochagua bima

0 comment 128 views

Namna sahihi ya kuendesha biashara yenye mafanikio ni pamoja na kuwa kujipanga kwa ajili ya hatari zozote zinazoweza kwani hakuna ambaye anajua matatizo yanayoweza kutokea katika biashara yake. Jambo moja ambalo kila mfanyabiashara anatakiwa kufikiria ni bima ili jambo lolote linatokea lisisababishe athari kubwa katika maendeleo ya biashara.

Kuna aina mbalimbali za bima ambazo zinatakiwa katika biashara. Ni muhimu kwa mfanyabiashara kufikiria kwa makini kabla ya kuamua ni bima gani inahitajika kwa ajili ya biashara yake. Baadhi ya mambo ya kuzingatia ni pamoja na haya:

Aina ya bima

Kuna aina mbalimbali za bima ambazo mfanyabiashara anaweza kutumia kwa ajili ya biashara zikiwemo ya moto, wizi, magari, mali na nyingine nyingi. Ni vyema kwa mfanyabiashara kuangalia bima yenye umuhimu na itakayofaa ili jambo lolote litakalotokea, lisuluhishwe kwa kupitia bima na kuondoa hasara. Kwa mfano kama wewe ni muuzaji wa gesi basi bima ya moto ni muhimu kwako kwa sababu ya hatari kubwa inayoweza kutokea ikiwa gesi zitashika moto.

Kuwa makini na kampuni feki

Kabla ya kulipia bima ni vyema kuhakikisha kuwa kampuni inatambulika na serikali na taasisi zote stahiki. Watu wengi wamepoteza fedha zao kwa kuchukua bima katika kampuni ambazo hazitambuliki na serikali na mamlaka husika. Hakikisha unaomba vielelezo vya kampuni hiyo ili kuwa na uhakika. Siku zote ni muhimu kufanya utafiti ili kupata matokeo bora. Katika upande wa bima ni vyema kulinganisha huduma za bima kutoka makampuni mbalimbali ili kujua kampuni ipi inatoa huduma bora zaidi, na inakidhi matakwa yako.

Hakikisha una nyaraka muhimu

Nyaraka ambazo unatakiwa kuwa nazo ili kuweza kupata bima katika kampuni hutegemeana na kampuni husika hivyo unaweza kuuliza ni nini wanahitaji kutoka kwako ili kuepusha usumbufu wowote. Baadhi ya nyaraka muhimu ambazo huhitajika na makampuni mengi ni pamoja na leseni ya biashara na nyaraka za usaili, hati ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN), nyaraka zinazoonyesha thamani ya biashara nk.

Washauri majirani katika biashara

Muda mwingine biashara yako inaweza isiwe na vitu hatarishi vinavyoweza kusababisha majanga lakini biashara zilizo karibu yako zinaweza kusababisha majanga. Sio vibaya kutoa ushauri kwa wafanyabiashara wa karibu kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ili kuhakikisha usalama kwako na wa watu wengine.

Bima ambazo hutumika zaidi na wafanyabiashara ni bima ya moto, majanga ya asili, wizi, afya, mali na magari. Baadhi ya kampuni zinazotoa huduma ya bima nchini ni pamoja na Alliance Insurance Corporation Ltd, Alliance Life Assurance Limited, Britam Insurance Tanzania Ltd, First Assurance, ICEA Lion General Insurance Company (T) Limited, Insurance Group of Tanzania Limited, Jubilee Life Insurance Company Limited, MO Assurance Company Limited, Milembe Insurance, National Insurance Corp. (T) Ltd, Metropolitan Tanzania Insurance Limited na Phoenix of Tanzania Assurance Co. Ltd.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter