Home FEDHA Dk. Kijaji ataka Wizara ya Fedha kuwajibika

Dk. Kijaji ataka Wizara ya Fedha kuwajibika

0 comment 118 views

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, amesema kuwa wafanyakazi wa wizara hiyo wanatakiwa kuwajibika kwa  kusimamia rasilimali fedha na makusanyo ya kiserikali katika maeneo yote nchini.

Ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambapo wakati wa mkutano huo waliadhimia kujadili bajeti ya wizara hiyo.

“Haiwezekani wewe nini mhakiki mali wa serikali katika eneo lako lakini hujui mapato halisi ya serikali kwenye eneo lako, basi utakuwa huna maana ya kuitwa mhakiki wa serikali” amesema Dk Kijaji.

Pia, ametaja majukumu ya Wizara ya Fedha  ni kuhakikisha kuwa utekelezaji wa maagizo ya serikali kwenye ukusanyaji wa mapato na matumizi ya rasilimali fedha yanasimamiwa kila eneo,  kuendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya ndani pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi, kuimalisha usimamizi na udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali.

Naye, katibu mkuu wa Wizara hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, Dk. Doto James, amesema kuwa kupitia kikao hicho watajadili kuhusu bajeti ya mwaka 2017/18 na utekelezaji wake na makadilio ya bajeti ya mwaka 2018/19.

Vilevile, ameongeza kuwa vikao hivyo vimekuwa na umuhimu sana katika wizara hiyo, hivyo wanategemea kuvifanya mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kujadili maswala ya ndani na nje ya wizara.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter