Na Mwandishi wetu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ametoa shukrani za dhati kwa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo hadi kufikia sasa uwekezaji wao katika miradi mbalimbali ya maendeleo umefikia jumla ya Sh trilioni 74.93. Dk. Mpango amesema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa JICA Shinichi Kitaoka ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Katika kiasi hicho cha fedha, asilimia 76.0 inahusisha ruzuku, asilimia 3.8 ni mikopo yenye masharti nafuu huku asilimia 20.1 ikienda kwenye usaidizi wa kiufundi.
Dk. Mpango amemuomba Rais wa Shirika hilo kuendelea kufadhili miradi ya nishati ya umeme, miundombinu,kilimo, uvuvi na afya ili kuongeza kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi kupitia viwanda kwani bila uwekezaji mkubwa katika umeme na miundombinu, sekta ya viwanda haiewezi kuendelea.