Home FEDHAMIKOPO Deni la Taifa linatisha

Deni la Taifa linatisha

0 comment 104 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema serikali itaendelea kukopa kwani deni la taifa ni himilivu na mahitaji ya uwekezaji bado ni makubwa.Waziri Mpango amesema hayo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameongeza kuwa japokuwa deni la taifa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka, deni hilo bado ni himilivu kwa vigezo vyote na mkakati wa serikali hivi sasa ni kuhakikisha mikopo yenye masharti nafuu inapewa kipaumbele.

Dk. Mpango pia amesema wanajipanga kuongeza mapato ya ndani ya serikali huku wakipunguza matumizi yasiyo ya lazima. Amesisitiza kuwa serikali lazima ipatiwe mikopo ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hadi kufikia Machi mwaka huu, deni la taifa lilikuwa zaidi ya Sh. 48 trilioni ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 16.3.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter