Home FEDHAMIKOPO Madeni HESLB sasa kulipwa kwa simu

Madeni HESLB sasa kulipwa kwa simu

0 comment 94 views

Kaimu Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Fidelis Joseph amesema wanaodaiwa na Bodi hiyo sasa wanaweza kulipa madeni kupitia simu zao za mkononi. Joseph amesema hayo wakati akizingumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, mfumo huo mpya wa malipo utamrahisishia mdaiwa kulipa muda na wakati wowote.

“Awali tulipokea maswali na maoni kwanini tusitumie teknolojia ya simu ya mkononi kuwezesha wadaiwa kulipa madeni yao. Leo tunapenda kuwataarifu kuwa serikali imeamua kuanzisha mfumo wa kutumia simu za mkononi”. Amesema Kaimu huyo.

Joseph amewaeleza waandishi wa habari kuwa, ili kutumia mfumo huo mpya ambao kwa kiasi kikubwa unaondoa kero za kupanga foleni benki, mdaiwa anapaswa kuwa na kumbukumbu namba ambayo inatolewa na Bodi hiyo. Ameongeza kuwa mara baada ya kufanya malipo, mdaiwa atapewa taarifa ya salio muda huo huo.

“Ukishakuwa na kumbukumbu namba unachukua simu yako ya kiganjani na kuingia kwenye huduma ya malipo ya serikali, ukibonyeza utapewa huduma ya kuweka kumbukumbu, namba ya Bodi ni 111 na utaweka namba yako na kuweka kiasi, tayari utakuwa ushalipa deni lako.

Akizungumza kuhusu hali ya marejesho, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kwa mwaka 2016/2017, HESLB ilikusanya Sh. 116 bilioni, mwaka 2017/2018 Sh. 181 bilioni zilikusanywa na kwa mwaka 2018/2019 tayari wamekusanya Sh. 123 bilioni kati ya Sh. 153 bilioni ambazo wanalenga kukusanya kabla ya mwaka wa fedha kumalizika.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter