Home FEDHA Dk. Mpango ataka mashirika yasiyotoa gawio kujitathmini

Dk. Mpango ataka mashirika yasiyotoa gawio kujitathmini

0 comment 120 views

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amewaagiza wakuu wa mashirika ya umma yasiyotoa gawio kwa serikali kujitathmini kama bado wanastahili wadhifa huo. Dk. Mpango amesema hayo wakati akifungua kongamano la kujadili jukumu la taasisi za umma katika utekelezaji wa sera ya viwanda ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

 

Dk. Mpango ameeleza kuwa, takribani mashirika 232 yanamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 huku mawili yakimilikiwa kwa asilimia 50, manne yakimilikiwa kwa zaidi ya asilimia 50 na yapo mashirika madogo 32 kwa ubia ambayo yanaweza kubadilika yakiunganishwa.

 

Waziri huyo ameongeza kuwa kati ya mashirika 34 yanayomilikiwa kwa asilimia 100 na serikali, 30 yameshindwa kutoa gawio kwa mwaka 2016/2017 huku mashirika mengine 20 kati ya 36 yanayomilikiwa kwa ubia na wawekezaji nayo yakishindwa kuwasilisha gawio serikalini.

 

Dk. Mpango ameweka wazi kuwa haridhishwi na mashirika yasiyotoa gawio serikalini na kuwataka wakuu wa mashirika hayo pamoja na bodi zao kujitathmini ili serikali iondokane na yale yasiyofanya vizuri na kuwawajibisha wahusika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter