Home FEDHA TPC kubadilisha fedha za kigeni

TPC kubadilisha fedha za kigeni

0 comment 104 views

Baada ya kufungwa kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Februali mwaka huu, Shirika la Posta Tanzania (TPC) limefungua vituo 20 vya ubadilishaji fedha hapa nchini. Mtendaji Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe, amesema hayo na kuongeza kuwa, vituo hivyo vitafunguliwa rasmi Machi 15 na ofisi 17 za posta zitaanza kutoa huduma hiyo hadi itakapofika mwisho wa mwezi huu.

“Ofisi za kubadilishia fedha zipo Posta Mpya, City Drive (Posta ya zamani), Kariakoo, Mtaa wa Libya,Kijitonyama, Oysterbay na uwanja wa ndege. Pia huduma zitatolewa mji mkongwe wa Zanzibar na Arusha”. Amesema Mtendaji huyo.

Pamoja na hayo, Mwang’ombe ameeleza kuwa watahakikisha huduma hiyo inapatikana katika mipaka yote nchini, huku wakiupa kipaumbele mkoa wa Arusha kufuatia athari waliyopata hivi karibuni.

“Tunazo fedha za kutosha kutoa huduma hizi na endapo tutaona kuna changamoto tutaomba watu wengine ambao tunashirikiana nao kutoa huduma za kubadilisha fedha za kigeni”. Amesema Mtendaji huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Biashara TPC, Mwanaisha Ali Said, amesema kuwa wamejipanga kuimalisha biashara hiyo kwa kuongeza ofisi kila mkoa,na katika mipaka yote nchini akitaja mikoa mingine itakayofanya biashara hiyo kuwa ni Mwanza,Kigoma, Shinyanga, Kilimanjaro, Tanga na Mbeya.

“Kutokana na uhitaji mkubwa wa maduka ya kigeni hapa Dar es salaam, tumeongeza muda wa kufanya kazi ambapo maduka yetu kuanzia Jumatatu hadi ijumaa yatafungua saa 2 hadi saa 12 jioni na kwa Jumapili yatafunguliwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana”. Amesema Meneja huyo.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter