Home FEDHA TRA Njombe yasaka wakwepa EFD

TRA Njombe yasaka wakwepa EFD

0 comment 106 views

Baada ya kufanya operesheni ya dharura ya ukaguzi wa mashine za kielektroniki za risiti (EFD), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Njombe imebaini kuwa idadi kubwa ya taasisi za shule, vituo vya afya pamoja na zahanati mkoani humo hazitumii mashine hizo.

Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi wa mashine hizo, Meneja wa TRA Njombe, Musib Shaban amesema mamlaka hiyo inatoa muda wa siku kumi na nne kwa taasisi hizo kununua mashine za EFD na ikishindikana, zitapigwa faini ya kuanzia Sh. 3 milioni hadi Sh. 4 milioni kwa kuisababishia hasara serikali.

Shaban ameeleza kuwa uchunguzi huo umegundua kuwa kumekuwa na ukwepaji mkubwa wa ulipaji mapato katika taasisi binafsi za shule na afya, hali ambayo amedai inakwamisha jitihada za serikali katika kukusanya mapato na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo .

Meneja huyo amesema kuwa wamiliki wengi wamekuwa wakikwepa kutumia EFD kwa madai ya kutokuwa na elimu sahihi juu ya matumizi ya mashine hizo katika taasisi zao, jambo ambalo meneja huyo amelipinga na kutaka wamiliki wa taasisi hizo kununua mashine hadi kufikia 01 Machi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter