Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh trilioni 24.11 sawa na ufanisi wa asilimia 97.4 ya lengo la kukusanya St trilioni 24.76 katiki kipindi cha mwaka wa fedha 2022/23.
TRA imesema makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 8.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Taarifa ya TRA inasema katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/23 (mwezi April 2023 hadi June 2023, TRA imekusanya kiasi cha Sh trilioni 5.69 sawa na ufanisi wa asilimia 91.1 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 6.24.
“Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la 1.6% ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2021/22,” imesema taarifa hiyo.