Home FEDHA Ubadilishaji fedha kutungiwa kanuni

Ubadilishaji fedha kutungiwa kanuni

0 comment 104 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni zinaandaliwa. Dk. Mpango amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, kanuni hizo zitawapa waombaji binafsi na taasisi muongozo na masharti muhimu ya kuomba leseni za kuendesha maduka hayo. Waziri Mpango amesema serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maduka mengi ya kubadilisha fedha kutumika katika ukwepaji mapato ya serikali na vilevile utakatishaji wa fedha haramu.

“Hivi karibuni serikali kupitia Benki Kuu (BoT) imeendesha zoezi la ukaguzi wa maduka yanayotoa hudumaya ubadilishaji fedha za kigeni lakini kumekuwa na tuhuma mbalimbali zilizotolewa za kudai uwepo wa ukiukwaji wa Sheria na haki kwa wamiliki hao jambo la kushangaza hakuna mmiliki yoyote wa duka aliyewasilisha malalamiko”. Ameeleza Dk. Mpango.

Ameongeza kuwa kanuni hizo zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara bila kuathiri sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla. Waziri Mpango pia amewaambia waandishi kuwa, BoT imechukua tahadhari kuendeleza huduma ya ubadilishaji fedha hapa nchini kwa kuhakikisha inatolewa na Shirika la Posta pamoja na benki zote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter